• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • v Kanda ya Maziwa Makuu barani Afrika yaahidi uwazi katika mchakato wa uchaguzi

  Nchi zilizo kwenye kanda ya Maziwa Makuu zimeahidi kuongeza uwazi katika mchakato wa uchaguzi ili kuimarisha amani, utulivu, ujumuishi na maendeleo endelevu.

  Afrika
  • Mgonjwa wa kwanza wa Ebola mjini Goma DRC afariki dunia 2019-07-17

  Mgonjwa wa kwanza wa Ebola mjini Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amefariki dunia. Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Carly Nzanzu amesema, mtu huyu alifariki jana njiani wakati akipelekwa Butembo kwa matibabu kwenye kituo cha matibabu ya Ebola.

  More>>
  China
  • Wawakilishi wa Afrika wasifu umuhimu wa kiujenzi wa China katika sekta ya amani na usalama 07-17 19:56
  Mkutano wa kwanza wa amani na usalama kati ya China na Afrika umefunguliwa tarehe 15 mjini Beijing, na kuhudhuriwa na mawaziri wa ulinzi na wanadhimu wakuu 15 wa majeshi kutoka nchi za Afrika zikiwemo Cameroon na Ghana, wajumbe waandamizi wa nchi 50 za Afrika na idara za ulinzi za Umoja wa Afrika, pamoja na wawakilishi wa jeshi la China. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe kutoka Afrika wamesifu mchango wa kiujenzi uliotolewa na China katika sekta ya amani na usalama.
  More>>
  Michezo
  • SOKA: Kombe la Kagame- Azam FC yaipiga T.P. Mazembe, yatinga nusu fainali
  Mabingwa watetezi, Azam FC ya Tanzania wamekuwa wa kwanza kutinga nusu fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki yajulikanayo kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya T.P Mazembe ya DR Congo jana kwenye uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali Rwanda.
  More>>
  Makala
  • Biashara kati ya China na nchi za nje yadumisha utulivu

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje ilifikia karibu dola trilioni 2.14 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo. Wakati uchumi wa dunia unadidimia na vitendo vya kujilinda kibiashara vinaongezeka, ni vigumu kwa China kupata matokeo hayo mazuri katika biashara ya nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako