Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2003-10-23 16:00:10    
Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI

cri

 

 

 

 

 

 

 

 

Idhaa ya Kiswahili ya CRI ilirusha matangazo yake ya kwanza hewani kuanzia Tarehe Mosi, Septemba mwaka 1961 kutokana na ushirikiano na juhudi kubwa za wafanyakazi wa China na wataalamu wa kigeni. Bw Ali Miraji Mpatani, alikuwa miongoni mwa wataalamu waafrika waliokuja kusaidia wakati idhaa hii ilipokaribia kutimiza mwaka mmoja. Mtaalamu Mpatani alishirikiana bega kwa bega na wafanyakazi wa China na wanafunzi kadhaa walioshiriki kazi ya idhaa hiyo kabla ya kuhitimu masomo, alitoa mchango usiosahaulika katika kuiwezesha idhaa hii iendelee.
    Matangazo ya idhaa hii ya kiswahili yanarushwa kila siku hewani kupitia masafa mafupi kuanzia saa 1:00 hadi 2:30 jioni; pia yanasikika nchini Kenya kupitia Idhaa ya kiswahili ya KBC saa 11:00 jioni kila siku; na yanarushwa hewani kwa kupitia Kampuni ya MIH ya Afrika ya kusini kuanzia saa 2:00 hadi 3:00 na kuanzia saa 5:00 hadi 6:00 jioni(saa za Afrika ya Mashariki).
    Katika idhaa hii, kuna Taarifa ya Habari (kila siku), Maelezo Baada ya habari (Jumatatu hadi Ijumaa ), vipindi vya Wapenzi wa Michezo(Jumatatu), Nchi yetu Mbioni(Jumanne), Elimu na Afya (Jumatano), Tazama China (Alhamisi), Klabu ya Utamaduni (Jumamosi), Sanduku la Barua (Jumapili), Salamu Zenu (kila siku), Kuwa nami Jifunze Kichina (Jumanne na Alhamisi), Ijue China (Alhamisi) pamoja na Sayansi na Teknolojia (Jumatano).
    Kuwatumikia wasikilizaji wake na kuongeza urafiki kati ya China na Afrika ni wajibu na jukumu la siku zote la Idhaa ya Kiswahili ya CRI. Matangazo ya idhaa hii yanalenga kusema ukweli na kuaminika, kujitahidi kuwawezesha wasikilizaji waielewe China na kuielewa dunia na kuwa ni kama daraja la urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika. Kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita, Idhaa ya Kiswahli ya CRI imeendelea vizuri na kupata mafanikio makubwa kutokana na uungaji mkono wa wasikilizaji wake, na huu umekuwa ni msingi wa kuandaa vizuri vipindi vinavyo wafurahisha wasikilizaji wake. Wafanyakazi wake wataendelea na juhudi kubwa na kutumia busara ipasavyo ili waweze kuboresha vipindi vyake.