Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-09-09 20:30:13    
Maandalizi ya walimu nchini China yaboreshwa

cri

    Tangu kuasisiwa kwa China mpya mwaka 1949, China imeandaa mamilioni ya walimu wa shule za msingi na za sekondari, ambao wanabeba jukumu la kutoa elimu ya msingi kwa watoto walio wengi kabisa duniani. Hivi sasa, mfumo wa kuwaandaa walimu wa madaraja mbalimbali umekwishaanzishwa nchini China. Kuanzia mwaka 1997 hadi 2003, vyuo vikuu vya ualimu nchini China kwa jumla vilikuwa vimewaandaa wanafunzi milioni 1.59 wenye shahada ya kwanza, na wanafunzi elfu 50 wenye shahada ya pili. Zaidi ya hayo, wanafunzi milioni 1.83 walihitimu masomo ya taasisi na shule za ualimu, na walimu wengine zaidi ya milioni moja na laki mbili wa shule za msingi na za sekondari walipewa mafunzo ya ngazi ya shahada.

    Mhusika wa idara ya maandalizi ya walimu ya wizara ya elimu ya China alisema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, mfumo wa kijadi wa kuwaandaa walimu umerekebishwa, vyuo vikuu visivyo vya ualimu pia vinaweza kutoa mafunzo ya ualimu. Mwaka 2003, vyuo vikuu 298 visivyo vya ualimu nchini China vilikuwa na wanafunzi laki 5.34 wa kozi ya ualimu, ambao walichukua asilimia 28.2 ya wanafunzi wote wa kozi ya ualimu nchini China.

    Zaidi ya hayo, mfumo wa kuwaandaa walimu nchini China pia umefanywa marekebisho ili kuinua kiwango cha utoaji mafunzo ya ualimu. Hivi sasa, idadi ya vyuo vikuu vya ualimu imeongezeka na kufikia 103 kutoka 74 ya mwaka 1997, ambapo idadi ya taasisi au shule zinazotoa kozi ya ualimu imepungua. Mageuzi yaliyofanywa katika miaka ya hivi karibuni katika mfumo wa masomo wa vyuo vikuu na elimu iliyomo ya mafunzo inayoelekea karne ya 21 imeanza kutekelezwa, mafanikio makubwa yamepatikana katika mageuzi ya mtindo wa maandalizi, kurekebisha mfumo wa masomo, kuingiza hali ya kisasa ya njia ya utoaji mafunzo na kuinua hali ya utaalamu kwa walimu.

    Kuanzia mwaka 1999, mradi wa kuendelea kuwaelimisha walimu wa shule za msingi na sekondari umetekelezwa nchini kote, ambapo walimu hodari elfu kumi wa shule za msingi na sekondari wamepewa mafunzo ya kitaifa , na kufanya matayarisho ya walimu nchini China kuingia katika kiwango kipya. Mwezi Septemba mwaka jana, wizara ya elimu ya China ilianzisha mpango wa mtandao wa elimu ya walimu. Katika miaka 5 ijayo mpango huo utaanza kutoa mafunzo mapya yanayowahusisha walimu wote wa shule za msingi na sekondari, kuwapa walimu hodari mafunzo ya kiwango cha juu zaidi ili kuinua viwango vya shahada vya walimu wa shule za msingi na sekondari na uwezo wao wa kutoa elimu yenye sifa bora.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya elimu, katika miaka ya hivi karibuni, hali ya sifa ya walimu wa shule za msingi na sekondari kwa ujumla imeinuka.

Idhaa ya Kiswahili 2004-09-09