Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-11 19:21:08    
Michezo ya riadha ya wakulima wa China

cri

    Kutokana na maendeleo ya uchumi na jamii ya China, wakazi wa vijijini wanaochukua kiasi kikubwa cha idadi ya watu nchini China wanastarehe maisha ya aina mbalimbali ya kiutamaduni kama walivyo wakazi wa mijini. Katika upande wa michezo ya riadha, wakulima wanaweza kufanya shughuli mbalimbali za michezo mwaka mzima, kama vile kurusha tiara katika majira ya chipukizi, kufanya mashindano ya kuendesha mitumbwi katika majira ya joto, kucheza dansi ya dragoni na simba katika majira ya kupukutika na kufanya mashindano ya aina mbalimbali ya kujiburudisha katika majira ya baridi.

    Urushaji tiara una historia ya miaka elfu moja hivi nchini China. Kila inapowadia majira ya chipukizi, wakulima hupenda kurusha tiara karibu na nyumba zao au mashambani. Sehemu nyingi nchini China zina tamasha la tiara, mji wa Weifang mkoani Shangdong na mji wa Yangjiang mkoani Guangdong ni maskani mawili ya tiara katika kaskazini na kusini nchini China. Bwana Liu Chaokai ni mkulima wa wilaya ya Yangdong, ya mji wa Yangjiang, mkoani Guangdong, alisema:

    "Watu wote wa kijiji chetu wanapenda kurusha tiara, katika kipindi cha tamasha la tiara lililopita, kijiji chetu kilitengeneza tiara chenye urefu zaidi ya mita 5 na kushiriki mashindano."

    Mashindano ya kuendesha mitumbwi katika majira ya joto ni mchezo wa kijadi wa riadha katika vijiji vya kusini mwa China. Mitumbwi hiyo hutengenezwa na ubao, ni mwembamba na mrefu, katika ncha ya mbele ya mtumbwi, hupambwa na kichwa cha dragoni, hivyo mtumbwi wa aina huo huitwa mtumbwi wa dragoni nchini China. Wakati wa mashindano, kwa kawaida kuna wapiga makasia 20, nahodha mmoja na mpiga ngoma mmoja. Mpiga ngoma ni mwongozi wa timu, anawaongoza wapiga makasia kudumisha mwendo wa aina moja na kudhibiti upesi wa mtumbwi kwa milio ya mapigo yake. Wakati bunduki ya utoaji amri ikilia, mitumbwi mingi inayopambwa na kichwa cha dragoni inaenda mbio chini ya mapigo ya ngoma, ambapo watazamaji walioko kwenye kando mbili wanapiga makelele kwa nguvu ya kuwahamasisha washiriki wote, hali hiyo ni ya kufurahisha watu wote.

    Bwana Luo Qiqing ni mkulima wa kijiji cha Longmen, cha mji wa Guilin, katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang wa Guangxi, ambaye pia ni kocha wa timu ya kuendesha mtumbwi ya kijiji chake. alisema:

    "Kijiji chetu kina familia zaidi ya 500, na wakazi zaidi ya 2000. kijiji chetu kina historia zaidi ya miaka 200 ya kuendesha mtumbwi wa dragoni. Katika wakati wa mapumziko, wanakijiji hupenda kuendesha mtumbwi, hata tunafanya mashindano kati ya wanavijiji."

 

    Tofauti na uendeshaji mtumbwi, kucheza dansi ya dragoni au simba ni mchezo wa kuburudisha zaidi. Kwa mfano, kucheza dansi ya simba, watu wawili wanajipamba kama simba, wanaruka ruka kwenye nguzo zinazokwenda juu na chini, na kufanya vitendo vya kuwashtusha watu. Kwa kuwa mchezo huo umeunganisha pamoja ustadi wa Gongfu, sarakasi na dansi za kichina, si kama tu una vitendo vya hatari, bali pia una maonesho mepesi, hivyo unafurahisha sana wakulima wa China. Katika mikoa ya Guangdong, Ghuangxi, Fujiang ya kusini mwa China, karibu kila kijiji kina timu ya kucheza dansi ya simba. China imeunda kwa umaalum shirikisho la dansi ya dragoni na simba ili kuendesha na kusawazisha shughuli mbalimbali za kucheza dansi ya simba na dragoni nchini kote, kuweka kipimo cha kisayansi na kuandaa mashindano ya ngazi mbalimbali.

    Katika kipindi cha mapumziko ya kilimo baada ya mavuno ya majira ya kupukutika, vijiji mbalimbali hufanya mashindano mbalimbali ya kujiburudisha. Muda si mrefu uliopita, mashindano ya michezo ya wakulima ya China yalifanyika mjini Yichuan, mkoani Jiangxi, mashariki mwa China.

    Michezo ya mashindano hayo ni kama mashindano ya kubeba mzigo kwa kupanda baiskeli, kupandisha mimea ya mpunga kwa mkono, kukimbia kwa kusukuma tairi ya mpira na kadhalika.

    Nchini China kuna baiskeli wengi zaidi, japokuwa sasa wakulima wengi wa China wamekuwa na pikipiki na magari ya kilimo, lakini baiskeli zingali ni vyombo muhimu vya uchukuzi wa masafa ya kati kati na ya karibu. Mashindano ya uchukuzi wa kupanda baiskeli yana viwango tofauti, kiwango cha chini kabisa ni kupanda baiskeli kwa kilomita 20 wakibeba mzigo wa kilogramm 30.

    Kupanda mimea ya mpunga kwa mkono ni kazi ya kawaida sana katika vijiji vya China, japokuwa hivi sasa wakulima wanafanya kazi hiyo kwa vyombo vya kilimo katika sehemu nyingi nchini China, lakini mashindano ya aina hiyo pia yanakaribisha sana wakulima.

    Inafahamika kuwa, michezo mingi ya mashindano hayo inaambatana na shughuli za kilimo, ambapo watazamaji wengi pia ni wakulima kutoka sehemu mbalimbali nchini China na wa kienyeji. Mkulima Li Baozhu alikwenda mahsusui kutazama mashindano hayo kwa umaalum kutoka sehemu yenye umbali zaidi ya kilomita mia moja, alisema kuwa mchezo wa kushindana kupandisha mimea ya mpunga una maana sana. akisema:

    Katika vijiji vya China, licha ya michezo ya riadha iliyotajwa hapo juu, michezo ya kisasa ya riadha kama vile mpira wa kikapu, uogeleaji na mpira wa meza pia inachezwa sana. Labda hali ya ushindani ya wakulima haiwezi kulingana na wachezaji maalum, lakini wanacheza kwa ajili ya kujenga afya, kujiburudisha na jambo linalofuatiliwa zaidi ni hali ya kusikilizana kati ya majirani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-11