Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-11-11 20:32:58    
Mafunzo ya kazi ni mbinu mpya bora ya kusaidia watu maskini

cri

    Mkulima kijana wa kijiji cha Luwan, wilaya ya Shanyang mkoani Shanxi Bw. Li Xiaochen, mwezi Aprili mwaka jana kutokana na msaada kutoka idara ya kusaidia watu maskini ya huko alipewa mafunzo ya kazi ya makanika kwa miezi 6 katika shule moja binafsi mjini Shangluo. Sasa amepata ajira katika mji wa Xian na anapata mshahara Yuan 1,500 kwa mwezi. Alimfundisha kaka yake mdogo ufundi huo, sasa pia amepata ajira na kuwa na mshahara Yuan 1,200 kwa mwezi. Katika muda wa mwaka mmoja tu, familia ya Bw. Li Xiaochen imeondokana na hali ya maskini.

    Wilaya ya Shanyang ni wilaya muhimu inayopewa msaada na serikali. Tokea mwaka jana, mkoa wa Shanxi ulifuata njia ya kusaidia familia maskini kwa kutoa mafunzo ya kazi ukilenga hasa kusaidia familia maskini zenye pato la chini ya wastani wa Yuan 865 kwa mwaka kwa kila mtu, na ada ya mafunzo inagharamiwa na serikali. Wanafunzi baada ya kuhitimu masomo wanapewa ajira kutokana na mapendekezo ya shule ya ufundi. Hivi sasa, familia nyingi za watu waliopewa mafunzo ya kazi wapatao zaidi ya 4,000 zimeondokana na hali ya umaskini kama familia ya Bw. Li Xiaochen. Uzoefu umethibitisha kuwa kuongeza sifa za ziada ya nguvu-kazi za vijijini katika sehemu maskini na kuhimiza uhamishaji wa nguvu-kazi kwa kupitia mafunzo ya kazi, siyo tu kuwa ni njia nzuri ya kusaidia familia maskini bali inapunguza shinikizo kwa mazingira ya asili, kuhimiza maendeleo ya viwanda na miji ya China na kufanya sehemu za vijijini zipate maendeleo.

    Kutokana na jitihada za miaka mingi, hivi sasa mkakati wa kusaidia familia maskini kuondokana na hali ya umaskini umepata mafanikio makubwa, hata hivyo bado kuna watu zaidi ya milioni 85 ambao hawajaondokana na hali ya maskini au wameondokana na hali ya maskini hivi karibuni tu. Idadi hiyo ya wakazi wanaishi katika mazingira duni, hivyo kuhamisha nguvu-kazi ni njia moja muhimu ya kuwasaidia kuondokana na umaskini. Kwa mujibu wa takwimu za baraza la serikali, hivi sasa nchini China watu zaidi ya milioni 13 kati ya watu milioni 85.17 wenye wastani wa pato la chini ya Yuan 882, wanatakiwa kuhamishiwa katika sehemu nyingine. Takwimu nyingine zilizotolewa na idara ya takwimu ya taifa zinaonesha kuwa ni 9% tu ya watu walipita mafunzo ya kazi kati ya watu milioni 480 wa sehemu ya vijijini. Hivi karibuni meya wa Dongguan wa mkoa wa Guangdong alitangaza kupitia televisheni kuwa mji huo hivi sasa unahitaji kwa haraka watu laki 2 au laki 3 wenye ujuzi fulani. Hali hiyo inaonesha kuwa bado kuna nafasi kubwa kwa uhamishaji wa watu wa sehemu ya vijiji, isipokuwa nafasi hiyo ni kwa wale wenye ujuzi. Idara husika za serikali zikitaka kuwasaidia watu maskini kwa kusafirisha nje nguvu-kazi hazina budi kuwaandalia mafunzo ya kazi ziada ya watu wa sehemu maskini.

    Upungufu wa vibarua uliotokea mwaka huu katika miji mingi ya China, siyo kuonesha ukosefu wa nguvukazi ya kimsingi, bali ni kuwa masoko ya ajira yanahitaji watu wenye ujuzi fulani badala ya kuhitaji watu wenye ujuzi wa msingi. Hayo ni mageuzi makubwa ya kihistoria katika soko la ajira kutokana na kubadilika kwa mtindo wa ongezeko la uchumi wa China. Usafirishaji nje wa nguvu-kazi kutoka sehemu maskini hauwezi kuwa wa kiholela, bali unapaswa kuwaandaa watu kwa mafunzo ya kazi kuendana na mabadiliko ya masoko ya ajira ili kutoa nguvu-kazi wanayohitajika watoe katika uzalishaji mali wa viwanda vya kisasa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-11-11