Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-02 18:56:54    
Kupika mahindi pamoja na punje za msonobari

cri

Mahitaji

Mahindi gramu 200, punje za msonobari gramu 30, maharagwe gramu 10, mafuta yaliyokwisha kuchemshwa gramu 500, chumvi nusu kijiko, M.S.G nusu kijiko, mafuta ya uto kijiko kimoja, kiasi kidogo cha maji ya wanga.

Njia

1. chemsha maji na tia mahindi ndani ya maji kwa dakika chache tu, kisha yapakue na uyakaushe.

2. Pasha moto mafuta mpaka yawe na joto la nyuzi 60 hivi, tia punje za msonobari, korogakoroga halafu tia mahindi, maharagwe, chumvi, M.S.G, korogakoroga mpaka mahindi yawe laini, mimina maji ya wanga, yakoroge na tia mafuta ya uto, pakua na sasa iko tayari kuliwa.