Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-06 16:54:46    
Jengo jekundu la Chuo kikuu cha Beijing na Jengo la Mlango wa Tian An Men.

cri

Beijing, mji mkuu wa China ni mji wenye historia ndefu, matukio mengi makubwa katika historia ya China yalitokea mjini Beijing, hivyo mjini Beijing yamejengwa majumba mengi ya makumbusho ya historia, Jengo jekundu la Chuo kikuu cha Beijing na Jengo la Mlango wa Tian An Men ni "mashahidi wawili maarufu wa historia".

Naona Jengo jekundu la Chuo kikuu cha Beijing lilikuwa na umaalum wake mkubwa katika wakati ule nchini China, jengo lenyewe linawavutia sana watu macho. Lakini historia yake muhimu inanivutia zaidi, kwani kutokana na historia yake naweza kuona historia ya China.

Hayo yalisemwa na mtalii aitwaye Lu Ailing. Jengo jekundu hilo liko katika mtaa wa Wusi No.29 katikati ya Beijing, ambapo ilikuwa sehemu ya zamani kilipokuwepo Chuo kikuu cha Beijing, na ofisi za chuo, maktaba na taasisi ya fasihi ya Chuo kikuu cha Beijing zote zilikuwepo hapo, jengo hilo pia lilikuwa chimbuko la harakati za Tarehe 4 Mei ya mwaka 1919. Jengo hilo jekundu lilisanifiwa na mtaalamu wa ujenzi wa Ureno, mtindo wake wa kiulaya ulionekana dhahiri, hivyo jengo hilo lilikuwa jengo la kisasa zaidi katika mji wa Beijing wa wakati ule. Chuo kikuu cha Beijing kilihamia sehemu ya magharibi ya Beijing miaka mingi iliyopita na kimekuwa chuo kikuu maarufu kabisa cha China, na Jengo jekundu limehifadhiwa kama mabaki ya kale ya taifa likiwa Jumba la makumbusho ya harakati za utamaduni mpya wa China.

Mtoa maelezo kuhusu jengo hilo Dada Duan Dongdong akifahamisha alisema:

Jengo hilo lilijengwa kwa matofali mekundu, hivyo watu walizoea kuliita Jengo jekundu.

Jengo hilo limekuwa kumbukumbu ya historia si kama tu kutokana na rangi yake bali pia kutokana na watu wengi waliofanya kazi na kusoma katika jengo hilo, ambao matumaini waliyotafuta na moyo walioutetea si kama tu viliathiri wanafunzi wa Chuo kikuu cha Beijing, bali pia viliathiri mwelekeo wa kusonga mbele kwa China, historia ya baadaye ilionesha hali hiyo. Naibu mkurugenzi wa Jumba la makumbusho ya Jengo jekundu Bibi Guo Junying alisema:

Jengo jekundu lilikifanya Chuo kikuu cha Beijing kuwa sehemu ya mkusanyiko wa fikra mpya, watu wapya na mawimbi mapya, na kukifanya kuwa Chuo kikuu kipya cha Beijing. Katika jengo hilo walikuwepo wasomi wengi wenye fikra ya kimaendeleo ambao walitafuta njia ya namna ya kuigeuza China, hivyo tunaona kuwa Jengo Jekundu ni jengo lenye alama ya zama za karibu za China, ambalo limeonesha kuwa China imesonga mbele kwa kuelekea zama za karibu tangu hapo.

Miongoni mwa watu wengi wa historia waliofanya kazi na kusoma katika Jengo jekundu, alikuwepo Mao Zedong ambaye baadaye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa China Mpya. Mao Zedong alikuwa msimamizi wa maktaba wa jengo hilo, kazi hiyo ilikuwa ya kwanza kwake tangu alipofika Beijing kutoka maskani yake. Chumba alichofanya kazi Mao Zedong wakati wa zamani bado kimehifadhiwa, ambacho kimeonesha historia halisi ya zamani.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-06