Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-08-08 17:34:34    
Kutembelea vichochoro vya mjini Beijing

cri

Vichochoro vya Beijing vilijengwa mapema katika karne ya 13, vingi vilikamilika katika enzi tatu za kale za China za Yuan, Ming na Qing. Katika enzi hizo, kwenye ujenzi wa mji wa Beijing, kasri la kifalme ni kiini cha ujenzi, makazi ya watu yalijengwa pembezoni mwa kasri la kifalme, na vichochoro ni njia nyembamba zilizotapakaa kati ya makazi ya raia.

Baada ya maendeleo na mabadiliko yaliyotokea katika karne kadhaa zilizopita, vichochoro vimetapakaa katika kila pembe ya mji mkongwe wa Beijing, ambavyo vinapishana kama mishipa kwenye mwili wa binaadamu. Vichochoro hivyo si kama tu vinahusiana na maisha ya kila siku ya wabeijing wengi, bali pia vimekuwa vivutio vya mji wa Beijing. Vichochoro hivyo vimejaa harufu nzito ya maisha ya makabwela. Watu wakitembea vichochoroni watajionea moja kwa moja historia na hali ilivyo ya sasa ya Beijing, na kuona maisha halisi ya wachina. Hivyo wabeijing wengi wanaona kuwa, kama wageni hawajawahi kutembea vichochoro vya Beijing ni vigumu kwao kuijua hali halisi ya Beijing, na kutoweza kutembea vichochoro vya Beijing ni jambo la kusikitisha.

Kampuni za utalii za Beijing pia zimetembeza shughuli zao za aina mbalimbali za matembezi kwenye vichochoro vya Beijing. Dada Yang ni msimamizi wa shughuli za matembezi ya vichochoro kwenye mtaa wa Xuanwu mjini Beijing alisema:

Watalii wakifika Qianmeng, wanaweza kupanda baiskeli zenye magurudumu matatu, mwongoza utalii anaweza kuwaongoza kutembelea vichochoro kadhaa vyenye mtindo maalum, ama vile vyenye historia ya miaka mia mbili au mia tatu ambavyo bado vimehifadhiwa kikamilifu, ambapo mwongoza wa utalii atawafahamisha hali kuhusu vichochoro hivyo vya Beijing, na kuwapeleka hadi nyumbani kwa wakazi kujionea maisha ya wakazi wa kawaida.

Watu wanaweza kutembea kwa miguu kwenye vichochoro mjini Beijing, au kupanda baiskeli zenye magurudumu matatu kuangalia hali halisi ya vichochoroni. Bwana Gunter Wein kutoka Ujerumani alisema kuwa, kupanda baiskeli yenye magurudumu matatu inayoendeshwa na mtu kwa nguvu yake, ni rahisi kwa mtalii kuangalia vizuri zaidi hali ya vichochoro. Akisema:

Nimewahi kuona baiskeli kama hiyo nchini India, baiskeli hiyo ni nzuri sana na inafaa zaidi kuendeshwa vichochoroni, na inaweza kuwaongoza watalii kwenda kila pembe ya kichochoro, lakini taxi haiwezi kufanya hivyo. Vichochoro vya Beijing ni kitu maalum cha Beijing, vikilinganishwa na majumba makubwa na marefu au sehemu za biashara, watalii wanavipendelea zaidi.

Watalii wakiwa na hamu kubwa juu ya maisha ya wakazi wa Beijing, wanaweza kutoa ombi la kwenda nyumbani kwa wakazi kunywa chai au kula chakula pamoja na wakazi. Bwana Zhang Shuo wa Shirika la utalii la kimataifa la China anatetea sana kuwapangisha watu wanaotaka kuishi kwa usiku mmoja nyumbani kwa wakazi wa Beijing alisema:

Watalii wakipata fursa ya kulala kwa usiku mmoja nyumbani kwa wakazi wa Beijing watafurahi zaidi, labda mwishoni mwa mwaka huu mpango huo unaweza kuanza kutekelezwa.

picha husika>>

1  2