Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-10 20:28:40    
Mandhari nzuri ya kimaumbile

cri

China ina rasilimali nyingi za maumbile, licha ya Jiuzaigou, Zhangjiajie na Huanglong, ambazo zimeorodheshwa kuwa mabaki ya kimaumbile ya dunia, kuna sehemu nyingine zenye mandhari nzuri ya kimaumbile zikiwa ni pamoja na Guilin ya sehemu ya kusini magharibi, milima ya Changbai ya sehemu ya kaskazini mashariki, milima ya Wasichana Wanne ya mkoa wa Guzhou na misitu ya sehemu ya joto ya Xishuangbanna ya mkoa wa Yuannan pamoja na mandhari ya misitu ya minazi ya kisiwa cha Hainan pia ni mandhari nzuri ya kimaumbile

MLIMA WA CHANGBAI

Mlima wa Changbai uko katika mkoa wa Jilin, sehemu ya kaskazini mashariki ya China, ambayo ni mpaka kati ya nchi za China na Korea ya kaskazini na chanzo cha mito mitatu ya Tumen, Yalu na Songhua. Misitu minene isiyo na upeo pamoja na ndege na wanyama adimu wanaoishi ndani yake, imefanya mlima huo kuorodheshwa kuwa hifadhi ya viumbe ya umoja wa mataifa duniani katika mwaka 1980. hivi sasa, mlima wa Zhangbai umethibitishwa kuwa sehemu ya mandhari nzuri ya taifa ya ngazi ya 4A.

Mlima wa Changbai ambao unajulikana kwa "mlima wa kwanza wa sehemu ya kaskazini mashariki", katika historia ulikuwa sehemu wanayokaa wakazi wa sehemu ya kaskazini mashariki, na pia ni sehemu ya kukua na kustawi kwa kabila la wa-man. Hivyo katika enzi ya Qing, sehemu hiyo ilichukuliwa kuwa ni sehemu takatifu. Mlima wa Changbai unajulikana duniani kwa mandhari nzuri ya utalii, sehemu na kustawi kwa kabila la waman na mlima mtakatifu wa kabila la wakorea.

Mlima wa Changbai unajulikana kwa kuwa na rangi nyeupe kutokana na aina ya mawe meupe ya floatstone na theluji zilizoko katika kilele chake kikuu. Mlima huo ni uliumbwa kutokana na volkano, kutokana na data kuwa mlima huo ulilipukao mara tatu toka karne ya 16. Sura ya ardhi ni nzuri ajabu. Mandhari nzuri za mlima huo ni pamoja na ziwa la mbinguni, misitu ya mbetula, msitu ulioko chini ya ardhi, misonabari warembo, bonde kubwa, bustani iliyoko juu ya mlima, kilele kikuu, chemchem, mlango wa upepo mweusi na msitu wa floatstone.

Mlima wa Changbai una mazao ya jadi ya gen-seng, ngozi za marten, pembe za paa, licha ya hayo mlimani kuna raslimali za viumbe adimu zikiwa ni pamoja na misonobari warembo, mizabibu na uyoga mwitu, maua ya azelia, chui mkubwa na korongo wenye kichwa mwekundu.

Mawasiliano ya kwenda mlima wa Changbai ni mepesi sana, unaweza kupanda ndege kutoka Beijing, Shanghai na Shenyang hadi mji wa Jianji, halafu kufika huko kwa magari. Kuna mahoteli ya ngazi mbalimbali chini na juu ya mlima, chumba kizuri ni Yuan za Renminbi 220 kwa siku, na kitanda kimoja cha kawaida ni yuan toka 10 hadi 40 kwa siku.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-10