Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-04-04 15:25:29    
Mapishi ya kamba-mwakaje na uyoga

cri

Mahitaji:

Kamba-mwakaje gramu 150, ute wa yai moja, uyoga gramu 50, mafuta gramu 200, mvinyo wa kupikia gramu 10, chembechembe za kukoleza ladha gramu 5, wanga gramu 15, maji ya wanga gramu 20, chumvi gramu 5, vipande vya vitunguu maji gramu 5, vipande vya tangawizi gramu 3.

Njia:

1. osha kamba-mwakaje, koroga pamoja na ute, chumvi na wanga, kata uyoga uwe vipande.

2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi ya 50, tia kamba-mwakaje, korogakoroga, halafu pakua. Tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, tia vipande vya uyoga, mimina mvinyo wa kupikia, chumvi na mimina maji kidogo, baada ya kuchemka, tia kamba-mwakaje, korogakoroga, punguza moto, tia chembechembe za kukoleza ladha, mimina maji ya wanga, korogakoroga, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.