Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-05-05 19:21:36    
Tovuti za kifamilia nchini China

cri

Kutokana na maendeleo ya uchumi na jamii, kompyuta kimekuwa ni kitu cha lazima kwa familia nyingi nchini China. Lakini hali ya watoto kupenda kucheza michezo kwenye kompyuta inawafanya wazazi wa watoto wengi waone usumbufu. Binti ya Bwana Hai Yang mwenye umri wa miaka 12 ni mmoja kati ya watoto hao. Lakini tofauti na wazazi wa watoto wengine ambao wanajitahidi kuwazuia watoto wao kucheza michezo kwenye kompyuta, Bw. Hai Yang alianzisha tovuti ya kifamilia na kumteua binti yake kuwa msimamizi mkuu wa teknolojia wa tovuti hiyo ili kumsaidia abadilishe ushabiki wake kutoka michezo ya kompyuta hadi kwenye shughuli nyingine zenye maana zaidi.

Binti wa Bwana Hai Yang anaitwa Hai Luo, ingawa binti huyo bado ni mdogo, lakini anashughulikia tovuti yake kwa makini, hivyo hana wakati wa kucheza michezo kwenye kompyuta. Alisema:

"Siku za kawaida naandika shajara, kujibu ujumbe unaotolewa na wageni kwenye tovuti, na kuongeza mambo mapya."

Xiao Hailuo ni hodari kujifunza mambo mapya, lakini baada ya muda mfupi, hamu yake ya kushughulikia tovuti hiyo ilipungua, baba yake alipoona hali hiyo alitafuta njia nyingine ya kumhamasisha, akafanya chombo cha kuhesabu idadi ya watu wanaotembelea tovuti hiyo na sehemu ya kutoa maoni. Mama yake Luo Ling pia alitoa maoni mara kwa mara kwenye tovuti yake ili kumpa moyo mtoto wake. Alisema:

"Mimi nilijifanya kama msomaji nikamwandikia ujumbe au kutoa maoni kwenye tovuti hiyo mara kwa mara ili kumhimiza aendelee na kazi hiyo yenye maana."

Hivi sasa kila siku Xiao Hailuo anajibu maoni ya wasomaji wake kwenye tovuti, au kuandika makala fupi. Alisema tangu tovuti hiyo ianzishwe, moyo wake wa kujiamini umeimarika, na uwezo wake wa kuandika makala pia umeongezeka. Bwana Hai Yang anafurahia kuona maendeleo ya binti yake katika kuandika makala. Mwaka uliopita Xiao Hailuo kwa jumla aliandika makala 15 zilizowekwa kwenye tovuti yao ya kifamilia, na kupokelewa kujiunga na shirikisho la waandishi watoto la mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China.

Bwana Hai Yang anafanya kazi ya elimu, maendeleo na mabadiliko ya binti yake yamemhamasisha kueneza uzoefu wake kwa wazazi wa watoto wengine ili kuwasaidia watoto wengi zaidi wawe na tabia nzuri ya kutumia kompyuta na kutembelea tovuti kwenye mtandao wa Internet. Mwaka 2005 Bwana Hai Yang aliishauri shule anayosoma Xiao Hailuo ianzishe shirikisho la tovuti za kifamilia, hivi sasa familia nyingi zimeanzisha tovuti zao za kifamilia.

"Familia mbalimbali zinaweza kuanzisha shughuli za aina mbalimbali za kijamii kwa kupitia shirikisho la tovuti za kifamilia, na watoto wanaweza kuwasiliana kwa kupitia tovuti hizo na kuunda kikundi cha watoto wakati wa likizo ili kujiburudisha wakati wa likizo."

Kwa kufanya shughuli hizo, watoto wamebadilisha kupenda kucheza michezo kwenye kompyuta hadi shughuli nyingine zenye maana zaidi. Si kama tu watoto wamepata nafasi ya kufundishana, wazazi wao pia wanaweza kuwasiliana kwa kupitia shirikisho hilo la tovuti za kifamilia, kubadilishana uzoefu na maoni kuhusu namna ya kuwaelimisha watoto.

Idhaa ya kiswahili 2007-05-05