Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2007-11-12 14:47:07    
Moja ya vipindi 24 katika kalenda ya kilimo ya China, Siku ya Kuanza kwa Majira ya Baridi

cri

Katika kalenda ya kilimo ya China kuna vipindi 24 kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini China. Tunaposema siku ya kipindi fulani tuna maana ya siku ya kuanza kwa kipindi hicho. Kugawa vipindi hivyo 24 katika kalenda ya kilimo ya China kunatokana na busara za Wachina wa kale na elimu yao ya unajimu, vipindi hivyo vinasaidia sana kupanga shughuli za kilimo. Kwa mujibu wa historia, mapema miaka zaidi ya 2000 iliyopita watu wa China walikuwa wamepata vipindi hivyo 24, yaani vipindi viwili kila mwezi.

"Siku ya kuanza kwa majira ya baridi" ni kipindi cha kwanza katika majira ya baridi, kipindi hicho huanzia tarehe 7 au 8 Novemba na kumalizika tarehe 22 au 23. Mwaka huu siku hiyo inaangukia tarehe 8 Novemba. Kabla ya kipindi hicho tulieleza kuhusu "Siku ya kuanza kwa majira ya Spring", "Siku ya kuanza kwa majira ya joto", na "Siku ya kuanza kwa majira ya Autumn", yote hayo yanamaanisha mabadiliko ya majira manne katika mwaka mzima.

"Siku ya kuanza kwa majira ya baridi" inamaanisha mwanzo wa majira ya baridi. Wahenga wa China walisema "siku ya kuanza" kwa kipindi fulani pia ni "siku ya mwisho" kwa kipindi kilichopita, lakini siku ya kuanza kwa majira ya baridi pia inamaanisha mwisho wa shughuli za kuvuna na kuweka mazao kwenye ghala, na tokea siku hiyo wadudu pia wameanza kujificha ardhini na kulala usingizi katika siku za baridi.

Kutokana na uchunguzi wa hali ya hewa, katika kipindi hicho upepo wa baridi kutoka kaskazini unaongezeka na kusababisha halijoto kupungua sana, hata mvua yenye theluji inaweza kunyesha.

Baada ya kuanza kwa siku ya majira ya baridi mimea huanza kukauka, na viumbe wanaanza kuacha shughuli zao ili kulimbikiza nguvu ya kujikinga dhidi ya baridi ili kuweza kuamka tena katika majira ya Spring mwaka kesho. Ingawa binadamu hawana tabia ya kulala usingizi katika majira ya baridi kama wadudu, lakini pia wanazingatia kulinda afya kwa chakula bora baada ya majira ya baridi kuanza. Kwa kawaida watu hula zaidi chakula kinacholeta joto mwilini hasa watu wanaoishi kaskazini magharibi mwa China wanakula zaidi nyama ya ng'ombe, mbuzi, matunda na mboga na chakula chenye vitamini nyingi. Hapo zamani China ilikuwa ni nchi ya kilimo, na "siku ya kuanza kwa majira ya baridi" ina maana ya kuvuna na kuhifadhi mazao, kwa hiyo watu waliofanya kazi mwaka mzima hupumzika na kula chakula kinono katika siku hiyo.

Jiaozi, chakula ambacho ni cha lazima kwa Wachina katika sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina, lakini pia ni chakula kisichokosekana katika "siku ya kuanza kwa majira ya baridi". Katika siku hiyo watu wa mji wa Harbin, mji uliopo kaskazini mashariki mwa China wana mazoea ya kufanya mashindano ya kuogelea wakifurahia majira ya baridi.

Idhaa ya kiswahili 2007-11-12