Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-10 17:33:43    
Bw.Issac Mbeche aeleza hali ya Chuo cha Confucius cha Nairobi

cri

Chuo cha Confucius ni taasisi ya elimu inayohimiza uenezi wa lugha ya Kichina na utamaduni wa China kote duniani. Hivi sasa kuna vyuo 271 vya Confucius katika nchi na sehemu 77 duniani, na idadi ya wanafunzi imefikia laki moja.

Chuo cha kwanza cha Confucius barani Afrika kilianzishwa mwaka 2005 katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Hadi hivi sasa vyuo 21 vya Confucius vimeanzishwa katika nchi 14 za Afrika.

Katika kipindi hiki, tunaye Bw. Issac Mbeche, mkurugenzi wa Chuo cha Confucius cha Nairobi, ambaye anaeleza hali ya chuo hicho, mafanikio kilichoyapata, changamoto zinazokikabili pamoja na mustakabali wa chuo hicho. Karibuni.