Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 14:58:05    
New York-Bw. Ban Ki-moon afuatilia sana hali mbaya ya kibinadamu inayoikumba Zimbabwe

cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 25 alitoa taarifa akieleza ufuatiliaji wake zaidi juu ya kuongezeka kwa idadi ya watu wenye njaa,kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu na hali mbaya ya kibanadamu nchini Zimbabwe, pia alihimiza mkutano kati ya vyama mbalimbali vya Zimbabwe uliofanyika siku hiyo nchini Afrika Kusini ufikie makubaliano kuhusu kuunda serikali mpya haraka.

Bw. Ban Ki-moon alisema, ana wasiwasi kuwa karibu nusu ya idadi ya watu milioni 12 wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa chakula, na kusikitishwa sana kutokana na kuzorota vibaya kwa huduma za matibabu na afya, mazingira na usafi na mambo ya elimu, na kuenea kwa haraka kwa maambukizi ya kipindupindu. Bw. Ban Ki-moon alitaka pande mbalimbali ziweke kando migongano ya kisiasa, na kuunga mkono na kutoa misaada ya kibinadamu.

Bw. Ban Ki-moon pia alihimiza vyama mbalimbali vifikie makubaliano kuhusu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.