• China ABC
  • Idhaa ya Kiswahili
  • Safari nchini China
  • Sanduku la barua
  • Uchumi
  • Jamii
  • China na Afrika
  • Utamaduni
  • Michezo
  • DJ Mosy
    Kama kipaji na utaalamu vingekuwa na jina lingine basi ingekuwa ni DJ MOSY ama Emanuel Moses Onasaa. Ni mzaliwa wa Africa ya mashariki mjini Dar es salaam nchini Tanzania. Bali ya kuwa na vipaji vingi Kijana huyu pia ni muwajibikaji sana katika kazi zake za usanii. Alipenda muziki tokea akiwa na umri mdogo na kumpelekea kujifunza zaidi kuhusu maswala ya muziki . Anaamini kwamba muziki ndio unaotufanya kufanikisha malengo yetu mengi kwenye maisha. Kwani muziki unatuburudisha, unatuliwaza, unatuelimisha, na pia unaweza kutuonya kwa yajayo. Na ndio maana yupo kukuletea kile kitakacho uburudisha moyo wako. Akiwa mitamboni hapa Radio chinia kimataifa kazi yake ni moja tuu, kuhakikisha unaburudika na kuelimika na yanyoendelea katika ulimwengu wa muziki.
    PK kama anavyojulikana mitamboni ni mtangazaji gwiji kabisa wa vipindi vya muziki hapa Radio China Kimataifa.Nimzaliwa wa Kenya na alijiunga nasi mwaka 2007.
    Kutana naye hewani kupitia 91.9 FM atakuletea kipindi muruwa kabisa cha muziki -Cheche zetu.Cheche zetu hujumuisha muziki kutoka bara Afrika pamoja na China.Kama anavyopenda kusema hewani, hii ni batobato ya wapenda kudansi na kusikiliza nyimbo za kila aina.
    Webradio
    Sauti
    2:00-3:00 asubuhi
    6:00-7:00 adhuhuri
    2:00-4:00 usiku
    Dira ya usikilizaji
    Maoni yako