• China ABC
  • Idhaa ya Kiswahili
  • Safari nchini China
  • Sanduku la barua
  • Uchumi
  • Jamii
  • China na Afrika
  • Utamaduni
  • Michezo
  • Mkutano wa baraza la Davos wafuatilia kama China inaweza kuiongoza dunia kukabiliana na msukosuko wa fedha

    (GMT+08:00) 2009-09-23 11:57:47

    Mkutano wa baraza la uchumi la dunia unaojulikana kama baraza la Davos la majira ya joto ulifanyika mjini Dalian, kaskazini mashariki mwa China kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 12 Septemba. Kwenye mkutano huo, maendeleo ya uchumi wa China na athari yake imekuwa suala ambalo limefuatiliwa na kujadiliwa na watu wengi kwenye mkutano huo.

    Kauli mbiu ya mkutano huo ni "kuhimiza tena ongezeko la uchumi". Wanasiasa, wafanyabiashara na wataalamu zaidi ya 1400 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 80 walihudhuria mkutano huo. Walifanya majadiliano kuhusu uvumbuzi, sayansi na teknolojia, uzalishaji, matumizi endelevu, fedha na uwekezaji. Mkutano huo umefanyika wakati ambao uchumi wa duniaunaonesha dalili ya kufufuka, hivyo mafanikio ya China katika kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani yamekuwa jambo linalofuatiliwa zaidi na watu waliohudhuria mkutano huo.

    Waziri wa uwekezaji wa Misri Dr. Mahmoud Mohieldin anaona kuwa mkutano huo si kama tu umewafahamisha watu hali ya uchumi duniani, bali pia umewafanya watu wa nchi mbalimbali wavutiwe na maendeleo ya China, akisema,

    "Kufanyika kwa mkutano wa baraza la uchumi la dunia hapa China kuna umuhimu mkubwa. Mkutano huo unaweza kusaidia watu wafahamu hali ya maendeleo ya uchumi. Hivi sasa mkutano huo umetoa mapendekezo kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China, na kutusaidia tuone mafanikio makubwa ya China, hivyo mkutano huo utanufaisha uhusiano wa pande mbilimbili kati ya China na nchi nyingine ikiwemo Misri."

    Sababu kubwa ya wanasiasa, wafanyabiashara na wataalamu wengi kuhudhuria mkutano huo ni kuwa watu wamepata moyo wa kukabiliana na msukosuko wa fedha kutokana na kufufua kwa uchumi wa China. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika tarehe 10, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alisema, hivi sasa uchumi wa dunia unafufuka hatua kwa hatua, na sera za China za kuchochea ongezeko la uchumi pia zimepata mafaniko. Hivi sasa China imezuia mwelekeo wa kushuka kwa ongezeko la uchumi, ongezeko la thamani ya uzalishaji nchini China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu lilikuwa asilimia 7.1, ongezeko la uwekezaji linaendelea kuzidi, mahitaji nchini yanaendelea kusukuma mbele ongezeko la uchumi, idadi ya watu wanaopata ajira mijini imeongezeka kwa milioni 6.66 kuanzia Januari hadi Julai, mapato ya wakazi wa mijini na vijijini yameinuka, na hali ya jamii ni tulivu. Mafanikio hayo yanatokana na mipango ya China ya kuchochea ongezeko la uchumi. Bw. Wen Jiabao alisema,

    "Wakati uchumi wa dunia unapodidimia sana, mafanikio hayo hayapatikani kwa urahisi. Serikali ya China na watu wake wamepata mafanikio hayo kwa kufuata hali halisi ya nchini China, kushikilia kutekeleza sera ya fedha iliyo mwafaka, kulegeza masharti ya sera za sarafu, na kutekeleza mipango mbalimbali ya kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani."

    Takwimu mpya zilizotolewa tarehe 10 na idara ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwelekeo wa kufufuka kwa uchumi wa China umeimarishwa, uwekezano wa kutimiza lengo la ongezeko la uchumi kufikia asilimia 8 katika mwaka huu umekuwa mkubwa zaidi.

    Lakini maendeleo ya uchumi wa China katika siku za usoni bado yataendelea kukabiliwa na changamkoto kubwa. Mustakabali wa uchumi wa dunia bado unakabiliwa na mambo mengi yasiyojulikana, shinikizo la kupungua kwa mahitaji ya bidhaa katika nchi za nje bado ni kubwa; kazi ya kupanua mahitaji nchini inakabiliwa na vizuizi vingi, uendeshaji wa viwanda na makampuni mbalimbali unakabiliwa na shida kubwa, kurekebisha miundo ya uchumi bado ni kazi kubwa na ngumu; ufanisi wa baadhi ya sera za kuchochea ongezeko la uchumi utapungua hatua kwa hatua, na baadhi ya sera zenye malengo ya muda mrefu bado zinahitaji muda wa kutimiza mafanikio. Hivyo Bw. Wen Jiabao alieleza kuwa katika hali hiyo China haiwezi na haitabadilisha sera zake, akisema,

    "Tutaendelea kuchukua kazi ya kuhimiza ongezeko kubwa la uchumi kwa utulivu kuwa kazi yetu ya kwanza, kushikilia kutekeleza sera ya fedha iliyo mwafaka, kulegeza masharti ya sera za sarafu, kufanya utekelezaji katika pande zote, kuboresha na kukamilisha mipango mbalimbali ya kuhimiza ongezeko la uchumi, kugundua na kutatua masuala mapya ya uendeshaji wa uchumi, kuzifanya sera zishughulikie mambo halisi, kuwa na ufanisi mkubwa na kuwa na sera endelevu. Pia tutatoa tahadhari na kuzuia hatari mbalimbali ambazo huenda zitatoekea zikiwemo mfumko wa bei, ili kutimiza ongezeko kubwa la uchumi wa China kwa utulivu na masikilizano na utulivu kwenye jamii."

    Hatua zilizochukuliwa na China wakati inapokabiliana na msukosuko wa fedha zinafuatiliwa na wafanyabiashara wengi duniani. mwenyekiti wa bodi na meneja mkuu wa kampuni ya Publicis ya Ufaransa Bw. Maurice Levy alisema, hatua zilizochukuliwa na China katika miaka ya karibuni ambazo zinalenga kuhimiza ongezeko la uchumi na kukabiliana na msukosuko wa fedha ni mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi mbalimbali. Bw. Levy alisema,

    "Sababu moja ya kuhudhuria mkutano huu ni kujifunza. Kwa sababu China imepata mafanikio makubwa katika kuhimiza ongezeko la uchumi. Mafanikio hayo hayaonekani katika nchi za magharibi. Nataka kujua kwa nini China imefanya vizuri namna hii na kupata mafanikio ya hivi sasa. Nimegundua sababu husika kwenye mambo ya uchumi. Pia nimegundua sababu husika kutoka kwa vitendo vya vijana na hatua zilizochukuliwa na serikali ya China. Mambo hayo yote yametupa funzo."

    Wakati utandawazi wa uchumi unaimarishwa siku hadi siku, nchi mbalimbali zimenufaika na maendeleo makubwa ya uchumi wa china naibu waziri wa uchimbaji wa madini wa Mongolia Bw. Zorigt Dashdorj alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, China ikiwa ni nchi ambayo inawekeza vitega uchumi vingi zaidi nchini Mongolia na mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Mongolia, ongezeko kubwa la uchumi wa China na mahitaji makubwa ya bidhaa yameipatia Mongolia fursa nyingi za maendeleo. Alisema Mongolia inapenda China na nchi jirani ziongeze uwekezaji nchini Mongolia, ili kuipatia nchi hiyo nafasi nyingi zaidi za ajira, na kuhimiza maendeleo ya viwanda nchini humo. Bw. Zorigt alisema,

    "Ongezeko la uchumi wa China pia limetupatia fursa nyingi. Tunatakiwa kufikiria kuongeza faida zetu, na kuyahimiza makampuni mengi zaidi ya Russia na China kuanzisha viwanda vya chuma na shaba nchini Mongolia, ili kutoa nafasi nyingi zaidi za ajira na kuhimiza maendeleo ya viwanda vya kisasa nchini mwetu."

    Uwezo mkubwa wa kufufuka kwa uchumi wa china umewafanya watu wengi waone kuwa China itaweza kuongoza dunia katika kuondoa msukosuko wa fedha. Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Sha Zukang alisema hivi sasa China bado haina uwezo huo, akisema,

    "Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, China bado ni nchi yenye mapato madogo. Bado ni vigumu kwa China kuongoza maendeleo ya uchumi wa dunia. Naona kuwa katika muda mrefu ujao, Marekani na Ulaya zitaendelea kuwa nguvu muhimu ya kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia."

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhang Xiaoqiang anakubali maoni hayo, akisema,

    "China ni nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Idadi ya watu nchini China inachukua moja ya sita ya idadi ya dunia. Thamani ya jumla ya uchumi wa China ni kubwa, ambayo ilifikia dola za kimarekani trilioni 4, na ongezeko la uchumi wa China litatimiza lengo la asilimia 8 katika mwaka huu. Kwa ukweli China itatoa mchango mkubwa zaidi katika kuchochea ongezeko la uchumi na jamii duniani. lakini China bado ni nchi inayoendelea ambayo wastani wa mapato ya watu wake ni mdogo. Hivyo bado tunahitaji muda mrefu kujiendeleza."

    Watu wengi waliohudhuria mkutano wa baraza la uchumi la dunia walisema mageuzi makubwa ya uchumi wa dunia yanafanyika, na mustakabali wa nchi mbalimbali unahusiana, hivyo zinatakiwa kufanya juhudi kushirikiana na kupata maendeleo pamoja.

    Webradio
    Sauti
    2:00-3:00 asubuhi
    6:00-7:00 adhuhuri
    2:00-4:00 usiku
    Dira ya usikilizaji
    Maoni yako