|
|
|||

Maonesho ya 6 ya bidhaa kati ya China na Umoja wa nchi za kusini mashariki mwa China ASEAN yalifungwa tarehe 24 Oktoba huko Nanning, China. Maonesho hayo ya siku tano yaliwavutia wafanyabiashara karibu elfu tano kutoka China, nchi wanachama wa Umoja wa ASEAN na nchi na sehemu nyingine duniani. Thamani ya biashara ya maonesho hayo ilikuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.6. Menesho hayo yamefuatiliwa na watu mbalimbali kwa kuwa eneo la soko huria kati ya China na Umoja wa ASEAN litaanzishwa mwanzoni mwa mwakani. 
Maonesho ya bidhaa kati ya China na Umoja wa ASEAN yanafanyika kila mwaka tokea mwaka 2004, na yametoa mchango mkubwa katika kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi mbalimbali za Umoja wa ASEAN. Makampuni ya nchi za umoja huo yanatangaza chapa zao na kuonesha bidhaa zao kwa wafanyabiashara wa China na nchi na sehemu mbalimbali duniani kupitia maonesho hayo. Kwenye maoensho ya mwaka huu, nchi 6 wanachama wa umoja huo zikiwemo Laos, Vietnam, Myanmar na Indonesia zilijenga mabanda yao ili kuonesha na kuuza bidhaa zenye sifaa ya kipekee.
Mfanyabiashara wa Myanmar Bw. Aung Naing ameshiriki kwenye maonesho hayo kwa mara nne, samani anazouza zinapendwa na wafanyabiashara wa China, na kila mwaka zinanunuliwa sana. Alisema,
"Maonesho hayo yanazidi kupata mafanikio, na yameyainufaisha makampuni, nchi na sehemu zinazoshiriki kwenye maonesho hayo. Si kama tu yanayasaidia makampuni yajulikane zaidi, bali pia yanayasaidia yaingie kwenye soko la kimataifa, hivyo maonesho hayo ni jukwaa la kupata mafanikio kwa pamoja. Eneo la biashara huria kati ya China na Umoja wa ASEAN litakapoanzishwa, litatunufaisha zaidi na kuleta fursa nyingi kwa mkoa wa Guangxi na Myanmar."
Mfanyabiashara kutoka mji wa Nanning mkoani Guangxi, China Bw. Mo Shanyi alishiriki kwenye maonesho hayo kwa mara ya kwanza. Kampuni yake inashughulikia utafiti na uvumbuzi wa teknolojia ya kubana matumizi ya nishati kwenye majengo na utengenezaji wa bidhaa husika. Bidhaa za kampuni hiyo zinapendwa na watu mkoani Guangxi. Bw. Mo anaona kuwa mkoa huo uko karibu na nchi wanachama wa Umoja wa ASEAN, na shughuli za ujenzi wa nyumba zinapamba moto katika nchi hizo, lakini teknolojia na wazo la kubana matumizi ya nishati bado halijaenezwa, hivyo kampuni yake ina fursa nzuri, akisema,
"Tumepanga kupanua soko letu katika nchi jirani. Tunafuatilia zaidi Vietnam na Thailand, kwa sababu hivi karibuni shughuli za ujenzi wa nyumba zinaendelezwa vizuri huko Vietnam, lakini miradi ya kubana matumizi ya nishati haijaendelezwa sana kama ilivyfanya China. Tuna matarajio makubwa kuhusu masoko ya nchi hizo."
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |