|
|
|||
Kombe la Dunia liliwasili nchini Kenya alhamisi na kupokelewa na rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Rais Kibaki alisema kuwasili kwa kombe hilo kuna umuhimu wa kihistoria, na kutaleta chachu kwenye shughuli za kuendeleza michezo nchini Kenya.
Alisema "kunyakua kombe la dunia ni ndoto ya kila mwanasoka na kuwasili kwake nchini Kenya ni fursa ya kutimiza tena malengo ya wanasoka na kuona kuwa ndoto hizo zinaweza kutimizwa"
Aidha, rais Kibaki aliwahimiza wanasoka vijana wanaotegemewa na wachezaji wa timu ya taifa Harambee Stars wawe na ndoto kubwa ili Kenya iwe nchi yenye nguvu kubwa kwenye mchezo wa soka.
Rais Kibaki alidokeza kuwa serikali imeunda kamati ya kushughulia mbinu za kuzialika timu nyingine ambazo zinacheza michezo ya kufuzu fainali za kombe la dunia kucheza mechi za kirafiki na Kenya, kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini.
Rais wa Kenya alisema kutokana na mtandao mzuri wa mawasiliano, ni rahisi kufika Kenya kutoka sehemu yoyote duniani na inachukua muda wa saa chache tu kutoka Afrika Kusini hadi Kenya kwa ndege.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |