• China ABC
  • Idhaa ya Kiswahili
  • Safari nchini China
  • Sanduku la barua
  • Uchumi
  • Jamii
  • China na Afrika
  • Utamaduni
  • Michezo
  • Matibabu ya jadi ya kichina yaonesha ufanisi katika kinga na tiba ya homa ya mafua ya aina ya H1N1

    (GMT+08:00) 2009-11-17 15:59:33

    Tangu mgonjwa wa kwanza wa homa ya mafua ya aina ya H1N1 agunduliwe nchini China, matibabu ya jadi ya kichina yametumika katika kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa huo. Katika kipindi ambacho maambukizi ya ugonjwa huo yameenea, wataalamu wa matibabu ya jadi ya kichina wametoa kanuni tofauti za dawa kwa makundi tofauti ya watu. Matokeo ya matibabu yamethibitisha kwamba matibabu ya jadi ya kichina yameonesha ufanisi mkubwa katika kinga na tiba ya ugonjwa huo.

    Katika shughuli za kukabiliana na homa ya mafua ya aina ya H1N1, matibabu ya jadi ya kichina yameendelea kuonesha uwezo wake maalumu. Mjumbe wa kikundi cha wataalamu wa matibabu ya ugonjwa huo katika wizara ya afya ya China na idara kuu ya usimamizi wa matibabu ya jadi ya kichina Bw. Liu Qingquan, alishiriki kwenye kazi za kutoa maelekezo ya matibabu kwa mgonjwa wa kwanza wa homa hiyo nchini China. Bw. Liu Qingquan alisema uzoefu wa kimatibabu umeonesha kuwa matibabu ya jadi ya kichina yana ufanisi mkubwa kwenye kutibu ugonjwa huo. Bw. Liu Qingquan alisema:

    "takwimu zetu zinaonesha kuwa wagonjwa waliotumia dawa za jadi za kichina homa yao ilishuka kwa haraka ndani ya siku 1 hadi 2 tu, dalili kubwa za ugonjwa huo zinaondolewa ndani ya siku 4 hadi 5, na baada ya wiki moja hivi wagonjwa wanapona. Dawa ya mitishamba ikilinganishwa na dawa ya Tamiflu, imeonesha ufanisi mkubwa zaidi katika kushusha homa, kuondoa kikohozi na maumivu ya kichwa, lakini katika kuondoa dalili kubwa za ugonjwa huo, dawa ya tamiflu ina ufanisi zaidi."

    Kwa mtizamo wa kimatibabu, homa ya mafua ya aina ya H1N1 ni ugonjwa unaotokea haraka lakini dalili zake si kubwa. Kwa mujibu wa nadharia za matibabu ya jadi ya kichina, ugonjwa huo unafanana na mafua yanayotokea wakati wa majira ya joto, yaani joto linaathiri mfumo wa kupumua na kusababisha dalili za homa na kukohoa. Matibabu ya jadi ya kichina yana uzoefu mkubwa kuhusu magonjwa ya aina hiyo. Kutokana na dalili za homa ya mafua ya H1N1, wataalamu waliweka mbinu maalumu ya kuondoa dalili za mafua za wagonjwa, mbinu hiyo si kama tu ina ufanisi mkubwa, bali pia ni salama zaidi na inaaminika.

    Hivi sasa baadhi ya nchi na sehemu duniani zimegundua virusi vinavyobadilika vya homa hiyo ambavyo vimekuwa sugu dhidi ya dawa ya Tamiflu, habari hiyo imefuatiliwa sana duniani. Licha ya hayo, athari mbaya ya dawa hiyo na upungufu wa akiba ya dawa hiyo duniani vyote vinahitaji utafiti kuhusu dawa ya mitishamba ya kichina iliyo salama, yenye ufanisi na ya bei nafuu. Mtaalamu Bw. Liu Qingquan alisema kanuni ya mseto ya dawa ya mitishamba ya kichina na ufanisi wake vinaweza kuepusha virusi kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo. Alisema:

    "kwanza dawa ya jadi ya kichina kwa kiasi fulani inaweza kuangamiza virusi, ya pili ni kwamba inaweza kuongeza uwezo wa viungo vya mwili hasa kurekebisha uwezo wa kujikinga dhidi ya magonjwa, ili kutimiza lengo la kutibu magonjwa. Dawa ya mitishamba haipambani moja kwa moja na virusi, inafanya kazi kwa malengo mengi, yakiwemo dalili za magonjwa na kuharibika kwa uwezo wa kinga ya mwili, na inatoa matibabu ya jumla dhidi ya magonjwa."

    Dawa za mitishamba zenye uwezo wa kupambana na virusi bado unaendelea, wataalamu husika wamejumuisha mpango wenye ufanisi wa kutibu homa ya mafua ya aina ya H1N1 kwa kutumia dawa ya jadi ya kichina. Idara husika ya afya imefikisha mpango huo kwa shirika la afya duniani.

    Katika kazi za kinga dhidi ya ugonjwa huo, dawa ya jadi ya kichina pia imeonesha umaalumu wake. Idara ya usimamizi ya matibabu na dawa ya jadi ya kichina hivi karibuni imetoa mpango wa kinga dhidi ya homa ya mafua ya H1N1 kwa dawa ya jadi ya kichina, ambao umeweka mpango rahisi pamoja na kanuni halisi ya dawa kwa makundi tofauti ya watu kujikinga dhidi ya ugonjwa huo. Mjumbe wa kikundi cha wataalamu wa matibabu ya ugonjwa huo katika wizara ya afya ya China na idara kuu ya usimamizi wa matibabu ya jadi ya kichina ya China Bw. Liu Qingquan alisema, kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hakuwezi kutegemea chanjo tu, dawa ya jadi ya kichina pia inaweza kufanya kazi yake maalumu. Bw. Liu Qingquan alisema:

    "dawa ya jadi ya kichina ina kinga dhidi ya mafua kutokana na hali ya mwili kwa watu tofauti, kwa mfano ni rahisi kwa watu wenye uwezo dhaifu wa kinga ya mwili kupata mafua. Tunatumia dawa za jadi za kichina kwa ajili ya kupunguza uwezekano wa kupata homa ya mafua. Aidha, kujikinga kwa njia ya kubadilisha mwenendo wa kula na wa maisha pia ni muhimu sana.'

    Webradio
    Sauti
    2:00-3:00 asubuhi
    6:00-7:00 adhuhuri
    2:00-4:00 usiku
    Dira ya usikilizaji
    Maoni yako