|
|
|||
Serikali ya Afrika ya Kusini tarehe 18 ilitangaza kuunda tume ya kupambana na ufisadi iliyoundwa na mawaziri, ili kupambana na vitendo vya ufisadi vya watumishi wa serikali.
Serikali ya Afrika ya Kusini ilitoa taarifa ikisema, vitendo vya ufisadi vimeathiri vibaya sura ya nchi hiyo duniani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tume hiyo itaundwa na mawaziri, kazi zao ni kufanya uchunguzi juu ya hali ya kila mtumishi wa serikali ambayo inahusika na vitendo vya ufisadi au la. Mwezi Januari mwaka kesho, tume hiyo itatoa ripoti moja na hatua za kupambana na ufisadi. Aidha, serikali ya Afrika ya Kusini ililaani vitendo vya ufisadi vilivyofanywa katika baadhi ya makampuni ya kibinafisi nchini humo.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |