|
|
|||
Mashindano ya sita ya kombe la balozi ya nyimbo za kichina yalifanyika tarehe 16 kwenye kituo cha utamaduni wa China cha Cairo nchini Misri. Kwa kupitia nyimbo za kichina, wanafunzi wa Misri waliimarisha uwezo wao wa lugha ya Kichina, pia walieleza upendo kwa China.
Wanafunzi 16 wanaosomea kozi ya lugha ya Kichina katika vyuo vikuu kikiwemo chuo kikuu cha Cairo na darasa la lugha ya Kichina la kituo cha utamaduni wa China cha Cairo, walishiriki kwenye mashindano hayo. Hayo ni ya mashindano ya sita ya nyimbo za kichina tangu kituo cha utamaduni wa China cha Cairo kianzishwe. Konsela wa ubalozi wa China nchini Misri anayeshughulikia mambo ya utamaduni, ambaye pia ni mkuu wa kituo cha utamaduni wa China cha Cairo Bi. Chen Dongyun alijulisha kuwa, hivi sasa mashindano hayo yamekuwa ni shughuli maarufu za kituo hicho. Alisema,
"Tunaboresha mashindano hayo kila mwaka. Kwa kuwa wanayafahamu mashindano hayo, hivyo kila mwaka wakati kama huu, wanaweza kufanya maandalizi na kushiriki kwenye mashindano hayo. Katika mashindano hayo ya mwaka huu, kiwango cha uimbaji ni cha juu zaidi kuliko zamani, hayo ni matokeo ya kujifunza lugha ya Kichina kwa wanafunzi hao, pia ni matokeo ya kazi za walimu wa Kichina na vijana wanaojitolea katika vyuo vikuu."
Bingwa wa mashindano hayo atapata fursa ya kutalii nchini China. Kutokana na msaada wa mwalimu wa lugha ya Kichina, mvulana Amr Kamel kutoka chuo kikuu cha Cairo alifanya maandalizi makubwa kwa ajili ya mengi kwa mashindano hayo. Ana matumaini kuwa atapata ubingwa, na kutimiza matumaini yake ya kutalii nchini China. Alisema,
"Nilifanya mazoezi mengi katika siku kadhaa zilizopita, nafurahi sana kwani ninaimba vizuri sana. Nataka kupata nafasi ya kwanza, ili nikatalii nchini China. Sizifahamu sehemu nyingi za China, lakini napenda kuzielewa."
Hatimaye msichana Raghda Alwy kutoka darasa la tatu la kozi ya Kichina la chuo kikuu cha Cairo alipata nafasi ya kwanza kwa kuimba wimbo uitwao "mkono mdogo na mkono mkubwa".
Raghda Alwy alifurahi sana, alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema,
"Nafurahi sana, nataka kwenda China, kwenda Beijing, hasa nataka kutembelea Mkuta mkuu. Sasa nitatimiza matumaini yangu."
Bolozi wa China nchini Misri Bw. Wu Chunhua aliangalia mashindano hayo. Alieleza matumaini yake kuwa shughuli kama mashindano hayo zitafanyika mara kwa mara nchini Misri, ili wamisri wengi zaidi waweze kuelewa utamduni wa China. Alisema,
"Mashindano hayo yalifanyika kwa mafanikio, na yamekuwa shughuli maarufu za kituo cha utamaduni wa China cha Cairo. Naona mashindano hayo yana umuhimu mkubwa, yanaweza kuhimiza kuenea kwa utamaduni wa China, na kufundisha lugha ya Kichina, hasa kuhimiza kuenea kwa nyimbo za lugha ya Kichina."
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |