|
|
|||

Bw. Hamid Karzai ameapishwa rasmi kuwa rais wa Afghanistan tarehe 19 huko Kabul, ambapo ameanza kipindi chake cha pili cha miaka nitano. Vyombo vya habari vinaona kuwa rais huyu atakabiliwa na changamoto kubwa katika kuboresha hali ya usalama, kuondoa umaskini na kupambana na ufisadi nchini humo katika miaka mitano ijayo.
Sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika siku hiyo kwenye ikulu ya Afghanistan, ilihudhuriwa na rais Asif Ali Zardari wa Pakistan, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi. Hilary Clinton na viongozi wa nchi nyingine. Balozi wa China nchini Afghanistan Bw. Zheng Qingdian amehudhuria sherehe hiyo akiwa kwa niaba ya serikali ya China.
Baada ya kuapishwa rais Karzai amesema anaitaka jumuiya ya kimataifa iendelee kuisadia Afghanistan katika ukarabati wa nchi, na kuyataka majeshi ya nchi nyingine nchini Afghanistan yapunguze vifo na majeruhi ya watu wa kawaida katika operesheni za kijeshi. Amesisitiza kuwa Afghanistan itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na Marekani, anatarajia Afghanistan itakuwa mshirika wa Marekani nje ya NATO.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |