|
|
|||
Tarehe 20 ni siku ya watoto duniani. Naibu mkurugenzi wa kamati ya kuwahudumia wanawake na watoto ya China Bibi Su Fengjie amesema kutokana na juhudi za miaka mingi, hali ya maendeleo ya watoto wa China imeboreshwa sana, ambapo hali ya afya, chakula, elimu ya watoto imefikia kiwango kilichowekwa na Umoja wa Mataifa kwenye Malengo ya Milenia.
Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa siku hiyo likishirikiana na Shirika la Habari la China, Xinhua, limetoa toleo la Kichina la ripoti ya Hali ya Watoto Duniani, ili kuadhimisha kutolewa kwa "Mkataba wa Haki za Watoto" miaka 20 iliyopita. Bibi Su Fengjie alipohudhuria sherehe hiyo alisema vifo vya waja wazito katika mwaka 2008 vilipungua kwa asilimia 67 vikilinganishwa na idadi ya mwaka 1989, huku vifo vya watoto wachanga pia vilipungua kwa asilimia 67 mwaka 2008 vikilinganishwa na idadi ya mwaka 1991. Mazingira wanayoishi watoto pia yameboreshwa zaidi, ambapo watoto wa familia maskini, watoto walemavu na watoto wa mitaani wanapewa matunzo maalum na serikali na jamii.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |