• China ABC
  • Idhaa ya Kiswahili
  • Safari nchini China
  • Sanduku la barua
  • Uchumi
  • Jamii
  • China na Afrika
  • Utamaduni
  • Michezo
  • Watu 42 wathibitishwa kufariki katika ajali ya mgodi wa makaa ya mawe

    (GMT+08:00) 2009-11-21 18:29:50
    Ajali ya mlipuko wa gesi iliukumba mgodi mmoja wa makaa ya mawe mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, tarehe 21 saa 8 na nusu usiku wa manane. Hadi siku hiyo jioni, miili ya wafanyakazi 42 imepatikana na wengine 66 bado hawajulikani walipo.

    Imefahamika kuwa wakati ajali hiyo inatokea, watu 528 walikuwa wakifanya kazi chini ya ardhi, na watu 139 miongoni mwao walikumbwa na ajali hiyo. Kati ya hao, watu 31 wameokolewa.

    Uchunguzi wa ajali hiyo umeanza, na matokeo ya mwanzo ya uchunguzi yanaonesha kuwa, chanzo chake ni ulimbizaji wa gesi nyingi kupita kiasi kwenye mgodi huo na kupelekea kulipuka.

    Rais Hu Jintao wa China na waziri mkuu Wen Jiabao wamemtaka naibu waziri mkuu Bw. Zhang Dejiang aende mahali ilipotokea ajali na kuongoza kazi ya uokoaji.

    Webradio
    Sauti
    2:00-3:00 asubuhi
    6:00-7:00 adhuhuri
    2:00-4:00 usiku
    Dira ya usikilizaji
    Maoni yako