|
|
|||
Mkutano wa mwaka 2009 wa baraza la ushirikiano na maendeleo ya viwanda kati ya China na Afrika umefunguliwa tarehe 21 hapa Beijing.
Mkutano huo umeandaliwa na shirika la ushirikiano wa viwanda la China, na kauli mbiu ya mkutano huo ni "usawa, uaminifu, ushirikiano na mafanikio ya pamoja". Maofisa wa serikali kutoka nchi zaidi ya 40 za Afrika na wajumbe zaidi ya 300 kutoka makampuni ya China na ya Afrika wamehudhuria mkutano huo, ambao wanaweza kujadili moja kwa moja biashara ya bidhaa za aina zaidi ya 100 na miradi zaidi ya 50 kwenye mkutano huo wa siku tatu.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la ushirikiano wa viwanda la China Bw. Gao Zongyin alisema, urafiki wa jadi kati ya China na Afrika ni mkubwa, ushirikiano kwenye sekta ya viwanda unasaidia kuhimiza na kuimarisha ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya pande hizo mbili, na kusaidia kuondoa athari ya msukosuko wa fedha kwenye makampuni ya China na Afrika.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |