|
|
|||
Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda walitia saini mkataba wa soko la pamoja la jumuiya hiyo tarehe 20 mjini Arusha,Tanzania, ili kutimiza utoaji wa huduma na biashara huria na watu kuweza kuvuka mpaka kutoka nchi moja hadi nyingine bila vizuizi katika sehemu hiyo.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania alisema kusainiwa kwa mkataba huo ni jambo la kihistoria, na jumuiya ya Afrika Mashariki itaendelea kusonga mbele kwenye mwelekeo wa utandawazi wa uchumi.
Soko hilo la pamoja linatarajiwa kuanzishwa mwezi Julai mwaka 2010, baada ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kupitisha mkataba huo nchini mwao.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |