|
|
|||
Hivi karibuni, Gazeti la Daily Post la Uingereza lilichagua wanasoka 50 bora zaidi wa Afrika, ambapo wachezaji wengi maarufu wamewekwa kwenye orodha hiyo wakiwemo Didier Drogba na Samuel Eto'O. Katika kipindi cha leo na wiki ijayo, tutawaeleza kuhusu wanasoka hao 50 waliozaliwa barani Afrika na kuchezea katika timu zao za soka za taifa.
50. El-Hadji Diouf

Akiwa mchezaji maarufu wa timu ya Senegal, Diouf aliisaidia timu yake kuingia robo fainali katika kombe la dunia lililoandaliwa kwa pamoja na Japan na Korea ya Kusini mwaka 2002. Diouf alianza kucheza soka nchini Ufaransa tokea utotoni mwake, aliwahi kuzichezea klabu za Sochaux na Rennes, lakini alijulikana sana baada ya kusajiliwa na timu ya Lens. Mwaka 2010 na 2012, Diouf alipewa tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa wanaume barani Afrika.
49. Emmanuel Amuneke
Amuneke ni mchezaji mwenye kipaji cha soka aliyeshindwa kutumia nguvu zake zote kutokana na kuwa na majeraha. Mwaka 1996, Amuneke alikwenda klabu ya Barcelona akitokea Madrid Atletico na kulipwa ada ya uhamisho paundi milioni 2.2. Akiwa mchezaji wa kiungo, mwaka 1996 Amuneke aliisadia timu ya soka ya taifa ya Nigeria kutwaa medali ya dhahabu kwenye michezo ya olimpiki ya Atlanta.
48. Peter Ndlovu

Zimbabwe siku zote iko daraja la tatu kisoka barani Afrika, lakini Peter Ndlovu ni mchezaji anayejulikana sana katika historia ya soka ya nchi hiyo. Mwaka 1991 aliichezea klabu ya Coventry, na mashabiki wa huko walipendezwa naye kutokana na ustadi wake wa kutoa pasi kwa wengine. Mtindo wake kupachika mabao kwa kumtia kiini macho golikipa kunaifanya timu ya Conventry isimame kidete kwenye soka nchini Uingereza. Akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambabwe, Ndlovu alishiriki kwenye mechi zaidi ya 100.
47. Papa Bouba Diop

Diop ni mchezaji mwengine maarufu wa Senegal, na alishirikiana na Diouf kucheza katika timu yake ya taifa kwenye michuano ya kombe la dunia la mwaka 2010. Akiwa mchezaji wa kiungo, Diop anajulikana kutokana na ustadi wake wa ulinzi katika eneo kubwa uwanjani.
46. Baddou Ezzaki
Kabla ya michuano ya kombe la dunia la mwaka 1986 kufanyika nchini Mexico, hakuna mtu aliyeweza kuitupia macho timu ya Morocco. Kwenye kombe la dunia la awamu hiyo, Ezzaki aliongoza timu ya taifa ya Morocco kufuzu kucheza robo fainali. Kwenye mechi za makundi, Morocco ilitoka sare na England na Poland, na kuicharaza Ureno.
45. Laurent Pokou
Kama si mchezaji Eto'o, Pokou bado angebaki kuwa ni mfungaji magoli mengi zaidi kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Mchezaji nyota Laurent Pokou alikuwa mshambuliaji mkali wa timu ya AS Nasy, na alijulikana sana kwenye soka nchini Ufaransa katika miaka ya 70 ya karne iliyopita. Rekodi yake ya kufunga magoli mengi zaidi kwenye kombe la dunia ilivunjwa na Eto'o miaka miwili tu iliyopita.
44. Steven Pienaar

Katika majira ya joto ya mwaka 2007, mshambuliaji wa Afrika Kusini Pienaar alihamia kwenye timu ya Everton akitokea Borussia Dortmund, ambapo alipata mafanikio makubwai. Hivi sasa, Pienaar anaaminiwa sana na meneja wa Toffees, Davod Moyes na uchezaji wake mzuri anapokuwa uwanjani unamfanya Pienaar apendwe sana na mashabiki wa Goodison.
43. Seydou Keita

Ada ya uhamisho paundi milioni 80 aliyopewa Keita imeonesha wazi wazi umuhimu wake kwa timu ya Barcelona. Akiwa mmoja kati ya kikosi cha timu ya Barcelona kilichopata ushindi wa vikombe sita, nguvu ya ushambuliaji na ulinzi wa Keita haiwezi kupuuzwa.
42. Thomas Nkono

Katika michuano ya kombe la dunia la mwaka 1982, timu ya Cameroon haikuingia kwenye muda wa mtoano, lakini kutofungwa mara tatu mfululizo kwenye mechi za makundi kuliifanya nguvu ya Cameroon isiweze kupuuzwa, hii inatokana na mchango mkubwa wa golikipa wa Cameroon Nkono. Mwaka 1979 na 1982 Nkono aliwahi kupewa tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.
41. Francois Omam-Biyik

Katika mechi ya ufunguzi ya kombe la dunia mwaka 1990 nchini Italia, mchezaji Biyik alipachika bao la ushindi kwa kichwa katika dakika ya 67 na kuifanya Cameroon iicharaze Argentina.
| © China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |