• China ABC
  • Idhaa ya Kiswahili
  • Safari nchini China
  • Sanduku la barua
  • Uchumi
  • Jamii
  • China na Afrika
  • Utamaduni
  • Michezo
  • Kikundi cha matibabu cha China kilichokwenda nchini Haiti charudi Beijing

    (GMT+08:00) 2010-02-10 10:14:42

    Baada ya kumaliza majukumu ya kutoa matibabu nchini Haiti, kikundi cha matibabu cha China kimefika leo kwenye uwanja wa ndege wa Beijing.

    Kikundi hicho kinaundwa na madaktari na wauguzi 40, ambacho kilifika Port-au-Prince tarehe 25 Januari na kuanza kutoa matibabu huko. Kilipokuwa nchini Haiti, kikundi hicho kiliwatibu majeruhi wapatao 4000, kutoa dawa na vifaa vya matibabu, na kutoa mchango mkubwa katika kinga na tiba ya ugonjwa baada ya tetemeko la ardhi.

    Tarehe 12 Januari tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.3 kwenye kipmo cha Ritcher lilitokea nchini Haiti, watu zaidi ya laki 2 walifariki, na wengine laki 2 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    2:00-3:00 asubuhi
    6:00-7:00 adhuhuri
    2:00-4:00 usiku
    Dira ya usikilizaji
    Maoni yako