• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya

 • Mkutano wa bunge la umma la China wafunguliwa
  More>>
  Habari
  • Rais wa China asisitiza kuwepo kwa utulivu mkoani Tibet 2012-03-09
  • China yafuata njia ya kujiendeleza inayolingana na hali halisi ya nchi 2012-03-09
  • Bunge la umma la China lathibitisha mswada wa marekebisho ya sheria kuhusu mashtaka ya uhalifu wa kijinai 2012-03-08
  • China yapenda kufanya ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika 2012-03-06
  • Rais Hu Jintao asisitiza kuimarisha kazi ya kuboresha maisha ya wananchi, afya na mfumo wa uhakikisho wa jamii 2012-03-05
  More>>
  Maelezo
  • Kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" chawekwa kwenye sheria ya mashtaka ya uhalifu wa jinai

  Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Bunge la umma la China unaofanyika sasa hapa Beijing, wameanza kujadili mswada wa marekebisho ya "Sheria ya mashtaka ya uhalifu wa jinai". Kwenye mswada huo, kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" kimeongezwa, na kinahusisha vipengele mbalimbali vya uandikishaji mashtaka, uchunguzi, kusikiliza kesi na kutoa hukumu. Wajumbe na wataalamu kuhusu haki za binadamu wanaona kuwa, marekebisho ya sheria hiyo yameonesha kuwa, mfumo wa sheria wa China unapata maendeleo makubwa siku hadi siku, na ni hatua kubwa katika mambo ya haki za binadamu nchini China.

  • China kuchagua wajumbe wa bunge la umma wa mijini na vijijini kwa uwiano sawa
  Mwaka kesho China itachagua wajumbe wa bunge la umma kwa kigezo sawa cha idadi ya watu mijini na vijijini, hii itawezekana kama rasimu ya uamuzi wa uchaguzi wa wajumbe iliyowasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura itapitishwa. Kwa mara ya kwanza idadi ya wajumbe 2000 wa bunge la 12 la umma itatolewa kwa maeneo ya mijini na ya vijijini kwa uwiano sawa. Uchaguzi wa wabunge wa bunge la 12 la umma utakamilika mwezi Januari mwaka kesho, miezi miwili kabla ya kwisha kwa kipindi cha bunge la 11 la umma.
  • Waziri wa biashara wa China akana lawama za Marekani kuhusu China kutofuata kanuni za WTO
  Hivi karibuni Marekani iliilaani China kuwa haifuati kanuni za Shirika la Biashara la Dunia WTO, na lawama zake hasa ni dhidi ya utoaji ruzuku wa China. Waziri wa biashara wa China Bw. Chen Deming amesema China siku zote inafuata kanuni za WTO, na kwamba serikali kuu ya China haitoi ruzuku zinazopigwa marufuku na WTO, na kama imetoa ruzuku kwa sehemu fulani, China inapenda kujadili jambo hili.
  • China yashikilia mkakati wa kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kunufaishana
  Waziri wa mambo ya nje wa China Yang Jiechi amesisitiza kuwa, miaka kumi ijayo itakuwa ni kipindi muhimu cha China katika kujipatia fursa za kimkakati za kujiendeleza. Amesema China itashikilia sera yake ya kidiplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia mambo, kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani na kutumia mkakati wa kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja.
  • Bunge la Umma la China lathibitisha kazi ya serikali
  Bunge la umma la China ambalo ni chombo chenye madaraka la juu zaidi cha China leo asubuhi limeitisha mkutano wake wa mwaka hapa Beijing, ambapo wajumbe karibu elfu 3 wamekusanyika katika Jumba la mikutano ya umma wakijadili mpango wa mwaka kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii.
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa
  Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China umefunguliwa rasmi leo hapa Beijing. Mkutano huo ni wa mwisho wa baraza hilo la awamu hii ya 11 ya muda wa miaka mitano.
  • Kuboresha maisha ya watu ni ajenda kuu katika mikutano miwili ya mwaka 2012 ya NPC NA CPPCC
  Mkutano wa mwaka 2012 ya Bunge la Umma la China na ule wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China itafunguliwa kwa nyakati tofauti kesho na jumatatu wiki ijayo hapa Beijing. Kuboresha maisha ya watu kumewekwa tena kwenye ajenda ya mikutano hiyo. Ugawaji wa mapato ya taifa, udhitibi wa bei ya nyumba na usawa wa kupata elimu pia vitafuatiliwa kwenye mikutano hayo.
  More>>
  Picha
  More>>
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako