• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuboresha maisha ya watu ni ajenda kuu katika mikutano miwili ya mwaka 2012 ya NPC NA CPPCC

    (GMT+08:00) 2012-03-02 17:56:00

    Mkutano wa mwaka 2012 ya Bunge la Umma la China na ule wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China itafunguliwa kwa nyakati tofauti kesho na jumatatu wiki ijayo hapa Beijing. Kuboresha maisha ya watu kumewekwa tena kwenye ajenda ya mikutano hiyo. Ugawaji wa mapato ya taifa, udhitibi wa bei ya nyumba na usawa wa kupata elimu pia vitafuatiliwa kwenye mikutano hayo.

    Takwimu mpya za serikali ya China zinaonyesha kuwa, mwaka jana thamani ya jumla ya uzalishaji GDP kwa kila mtu kwenye miji mikubwa ya Shanghai, Beijing na Hangzhou imefikia zaidi ya yuan elfu 80, ambayo ni sawa na dola za kimarekani elfu 12. Kiasi hicho kinakaribia kiwango katika nchi zilizoendelea kilichowekwa na Benki ya Dunia. Lakini, wananchi katika miji hiyo wanafuatilia kuhusu kuongezeka kwa gharama ya maisha, bei ya nyumba na ubora wa chakula.

    Xiao Yu amefanya kazi mjini Beijing kwa zaidi ya miaka miwili, na anasema haridhiki maisha yake katika mji mkuu:

    "nimefanya kazi kwa miaka miwili, lakini nina akiba ndogo kwani natumia pesa nyingi kulipia usafiri na kodi za nyumba. Ni matumaini yangu kuwa, katika miaka michache ijayo, nitaongezewa kipato changu na kuweka akiba zaidi."

    Zhou Qingjie ni profesa wa uchumi katika chuo kikuu cha teknolojia na biashara cha Beijing. Anasema ongezeko la GDP halina maana ya kuongezeka kwa furaha ya mtu. Akisema:

    "Si sahihi kulinganisha GDP na furaha. GDP inatumika kupima uzalishaji wa nchi kwa mwaka, bila kujali uchafuzi wa mazingira, ubora wa bidhaa na ubora wa chakula, pengo kati ya tajiri na maskini, wala haiangalii muda wa mtu kupumzika."

    Mwaka jana, pato la mtu mmoja mmoja katika miji nchini China liliongezeka kwa asilimia 8.4, na kwa mtu wa kijijini liliongezeka kwa asilimia 11.4 kuliko mwaka 2010. Lakini kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu na msingi dhaifu wa uchumi nchini China, ongezeko hilo la mapato haliwezi kukidhi matarajio ya watu wengi.

    Serikali kuu ya China inasisitiza kuwa itaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha maisha ya watu.

    Yu Jianrong ambaye ni mtafiti katika taasisi ya utafiti wa kilimo ya China, anasema serikali za mitaa zinapaswa kufanya kazi kubwa katika jambo hilo. Anasema:

    "Serikali kuu ilitunga sera, na serikali za mitaa zinapaswa kuitekeleza. Kwa mfano sasa tunafanya mageuzi ya kitambulisho cha ukaazi, watoto ambao wazazi wao ni wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini wanaweza kupata maisha na elimu sawa na watoto wa mijini."

    Wataalamu wanasema kuboresha maisha ya watu ni kazi muhimu sana inayohusu utulivu wa jamii. Hii ni mada inayostahili kujadiliwa kstika mikutano miwili ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako