• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2012-03-03 18:20:59

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China umefunguliwa rasmi leo hapa Beijing. Mkutano huo ni wa mwisho wa baraza hilo la awamu hii ya 11 ya muda wa miaka mitano.

    Mikutano miwili ya Bunge la umma la China na Baraza la mashauriano ya kisiasa inafanyika kila ifikapo mwanzoni mwa mwezi Machi. Leo wajumbe wapatao karibu 2200 wa Baraza la mashauriano ya kisiasa wanakusanyika hapa Beijing, ambapo watatoa maoni na mapendekezao yao mbalimbali kuhusu sera muhimu zinazohusu sekta mbalimbali za siasa, uchumi na maisha ya jamii. Maoni na mapendekezo yao yatawasilishwa moja kwa moja kwa serikali kuu ili kusaidia serikali kutoa maamuzi.

    Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa Bw. Jia Qinglin ametoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Halmashauri ya kudumu ya baraza hilo, akisema:

    "Katika mwaka mmoja uliopita, Baraza la mashauriano ya kisiasa limetoa mchango mkubwa katika kutekeleza kwa makini mashauriano ya kisiasa, kufanya usimamizi wa kidemokrasia, kutoa maoni na mapendekezo, kuwashirikisha watu wenye ujuzi kutoa huduma kwa maendeleo ya nchi, kujitahidi kuratibu uhusiano kati ya pande mbalimbali ili kuhimiza masikilizano ya jamii, na kutumia nguvu yake bora katika kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya utamaduni."

    Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa kwanza kwa China kutekeleza mpango wa 12 wa maendeleo ya miaka mitano ya uchumi na jamii, ambapo kuhimiza kazi ya kujiendeleza kwa njia ya kisayansi na kubadilisha njia ya kujipatia maendeleo ya uchumi ni kazi kuu katika utekelezaji wa mpango huo. Bw. Jia Qinglin anasema:

    "Wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa wametoa mapendekezo 6076 kuhusu kuimarisha marekebisho na udhibiti wa jumla wa maendeleo ya uchumi, kupanua mahitaji katika soko la nchi, kuboresha mwundo wa shughuli, kuendeleza kilimo cha kisasa, kusukuma mbele uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na kuendeleza kwa kina mageuzi na ufunguaji mlango. Maoni na mependekezo yao mengi yamesikilizwa na kuandikwa kwenye mipango mbalimbali maalum pamoja na nyaraka za sera."

    Kuhusu kazi ya baraza hilo katika mwaka 2012, Bw. Jia Qinglin amesisitiza katika ripoti yake akisema:

    "Baraza hilo ni lazima kuichukua kazi ya kuhimiza kujiendeleza kwa njia ya kisayansi kuwa kazi kuu ya baraza hilo, ambapo litaitisha mikutano mbalimbali kutoa nguvu kubwa ya kuendeleza shughuli halisi za uchumi, na kudumisha utulivu na maendeleo ya kasi ya uchumi. Baraza hilo litajitahidi kushirikisha nguvu za pande mbalimbali kutoa maoni na mapendekezo katika kuhimiza masikilizano ya jamii, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kujenga jamii yenye maisha bora kote nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako