• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa bunge la umma la China wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2012-03-05 09:24:40

    Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa baraza la 11 la bunge la umma la China umefunguliwa leo asubuhi hapa Beijing, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo rais Hu Jintao, spika wa bunge hilo Bw. Wu Bangguo, na waziri mkuu Bw. Wen Jiabao.

    Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao ametoa ripoti kuhusu kazi ya serikali kwa wajumbe karibu 3,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini China. Ripoti hiyo imekumbusha kazi ya serikali katika mwaka 2011, na mpango wa  kazi kwa mwaka 2012.

    Katika mkutano huo utakaofanyika kwa siku tisa na nusu, wajumbe watajadili ripoti hiyo ya kazi ya serikali, ripoti ya kazi ya halmashauri ya kudumu ya bunge la umma, ripoti ya kazi ya mahakama kuu, na ile ya idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka, ripoti kuhusu mpango wa kazi na bajeti ya serikali kwa mwaka huu, na maswala mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako