• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Hu Jintao asisitiza kuimarisha kazi ya kuboresha maisha ya wananchi, afya na mfumo wa uhakikisho wa jamii

    (GMT+08:00) 2012-03-05 10:43:38

    Rais Hu Jintao wa China jana amesema China inapaswa kuendelea kuhakikisha na kuboresha maisha ya wananchi, kusukuma mbele mageuzi katika mfumo wa matibabu na huduma ya afya, na kuharakisha ujenzi wa mfumo wa uhakikisho wa jamii unaohusisha wananchi wote.

    Rais Hu amesema hayo kwenye mkutano wa vikundi wa baraza la mashauriano ya kisiasa, aliposhiriki kwenye majadiliano na washauri kutoka sekta za afya, ustawi wa jamii na uhakikisho wa jamii. Ameseisitiza kuwa, serikali ya China inapaswa kufanya kazi ya uongozi katika kutatua matatizo makubwa zaidi yanayohusiana na wananchi moja kwa moja, na katika upande mwingine, ni lazima jamii nzima iongozwe ili kutekeleza desturi ya China ya kuwasaidia watu wenye uwezo mdogo, ili kuwafanya wawe na maisha mazuri zaidi. Rais Hu pia alisisitiza kuwa, China inabidi kuboresha mfumo wa huduma ya afya kwa jamii yote, kuharakisha na kuboresha mfumo wa uhakikisho wa jamii unaohusisha watu wa mijini na vijijini, na vilevile unaowahusisha walemavu. Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa Bw Jia Qinglin pia alishiriki kwenye majadiliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako