• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Umma la China lathibitisha kazi ya serikali

    (GMT+08:00) 2012-03-05 19:02:51

    Bunge la umma la China ambalo ni chombo chenye madaraka la juu zaidi cha China leo asubuhi limeitisha mkutano wake wa mwaka hapa Beijing, ambapo wajumbe karibu elfu 3 wamekusanyika katika Jumba la mikutano ya umma wakijadili mpango wa mwaka kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii.

    Waziri mkuu Wen Jiabao ametoa ripoti ya kazi ya serikali kwa niaba ya Baraza la serikali. Anasema: "Huu ni mwaka muhimu wa kuanza kutekeleza mpango wa 12 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii, pia ni mwaka wa mwisho kwa serikali ya awamu hii. Tunapaswa kutekeleza kwa makini majukumu yetu, kupiga hatua na kusonga mbele bila kuogopa taabu na bila kulegea, ili tupate mafanikio ya kuwaridhisha wananchi."

    Ripoti hiyo imetoa malengo makuu ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China kwa mwaka 2012, ambayo ni kuongeza thamani ya jumla ya uzalishaji mali nchini kwa asilimia 7.5; kuongeza nafasi za ajira mijini kwa zaidi ya milioni 9, na kudhibiti kiwango cha ukosefu wa ajira mijini ndani ya asilimia 4.6. Pia kudhibiti kiwango cha upandaji wa bei za matumizi ya wakazi ndani ya asilimia 4; kuongeza thamani ya jumla ya uuzaji na uagizaji wa bidhaa kwa asilimia 10, na kuendelea kuboresha hali ya mapato na matumizi ya serikali katika dunia.

    Kiwango cha ongezeko la thamani ya jumla ya uzalishaji mali nchini kilipungua kuwa asilimia 7.5 kutoka asilimia 8 mwaka jana. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya awamu hii kushusha kiwango hiki hadi chini ya asilimia 8. Kuhusu mabadiliko hayo, Bw. Wen Jiabao anafafanua:

    "Napenda kufafanua zaidi kwamba, kushusha kiwango hiki hasa ni kwa ajili ya kulingana na malengo ya mpango wa 12 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii, ili kuzielekeza pande mbalimbali ziweke mkazo katika kuharakisha kazi ya kubadilisha njia ya kujipatia maendeleo ya uchumi na kuinua kihalisi sifa na ufanisi wa maendeleo ya uchumi, ili kupata maendeleo ya muda mrefu zaidi, ya kiwango cha juu zaidi na yenye sifa nzuri zaidi."

    Katika ripoti yake, Bw. Wen Jiabao amesema bila kuficha kwamba, maendeleo ya uchumi na jamii ya China bado yanakabiliwa na taabu na changamoto nyingi. Mchakato wa ufufukaji wa uchumi wa dunia bado unaendelea polepole na unakumbana na changamoto nyingi, na msukosuko wa fedha bado unaendelea, huku msukosuko wa madeni katika baadhi ya nchi hauwezi kudhibitiwa ndani ya muda mfupi. Nchini China, kazi kubwa zaidi zenye changamoto ambazo zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka ni kuondoa migongano ya muundo wa mfumo, kupunguza hali isiyo ya uwiano katika maendeleo, na kutimiza maendeleo endelevu, huku matatizo mengi mapya yakitokea katika uendeshaji wa uchumi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako