• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kufanya ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika

    (GMT+08:00) 2012-03-06 14:30:01

    China inapenda kufanya ushirikiano na nchi mbali mbali za Afrika katika kujenga kwa pamoja siku nzuri za baadaye.

    Ameyasema hayo leo  waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi alipoongea na waandishi wa habari wa mkutano wa 5 wa wajumbe wote wa baraza la 11 la bunge la umma la China. Amesema China inaona fahari kuwa watu wa Afrika wanaichukulia China kuwa mwenzi wao wa dhati wa kufanya ushirikiano, China ni nchi inayoendelea, inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali za Afrika katika kujenga kwa pamoja siku nzuri za baadaye.

    Aidha Bw. Yang amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuunga mkono kwa pamoja nchi za Afrika katika juhudi zao za kujipatia amani na maendeleo, kuongeza uwezo wa kujiendeleza kwa kujiamulia, na kufanya kazi zaidi za kulinda haki na maslahi yao katika mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako