• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashikilia mkakati wa kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kunufaishana

    (GMT+08:00) 2012-03-06 18:13:48

    Waziri wa mambo ya nje wa China Yang Jiechi amesisitiza kuwa, miaka kumi ijayo itakuwa ni kipindi muhimu cha China katika kujipatia fursa za kimkakati za kujiendeleza. Amesema China itashikilia sera yake ya kidiplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia mambo, kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani na kutumia mkakati wa kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja.

    Bw. Yang Jiechi amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing wakati mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China ukiendelea.

    Alipozungumzia kazi kuu ya mambo ya kidiplomasia ya China kwa mwaka huu Bw. Yang alisema,

    "Kazi kuu ya mambo ya kidiplomasia ya China kwa mwaka huu ni kutoa huduma bora kwa ajili ya China kubadilisha njia ya kujiendeleza kiuchumi, kukabiliana vizuri na hatari na changamoto mbalimbali kutoka nje, ili kuweka mazingira mazuri zaidi ya nje kwa ajili ya China kujipatia maendeleo ya uchumi na jamii. Tutalinda kithabiti mamlaka na usalama wa nchi yetu, kuwa na juhudi zaidi kutetea kufanya mazungumzo na mashauriano kwa kutatua matatizo ya kimataifa na kikanda, haswa masuala yanayofuatiliwa zaidi duniani, ili China ioneshe umuhimu wa nchi kubwa inayowajibika na mambo. Aidha, tutaendelea kuimarisha urafiki na ushirikiano na nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa na kikanda, kuzidisha maslahi ya pamoja na kukabiliana kwa pamoja na changamoto mbalimbali za kimataifa, ili kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo kwa pamoja."

    Bw. Yang Jiechi amesema miaka kumi ijayo ni kipindi muhimu kwa China kujiendeleza kwa amani. China, ikiwa ni nchi inayoendelea, itashikilia sera ya kufungua mlango na kufanya ushirikianio wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja. Akisema,

    "katika miaka kumi ijayo, katika hali ya utandawazi wa uchumi wa dunia, pande mbalimbali zitazingatia zaidi kubadilisha njia ya kujiendeleza kiuchumi, kufanya juhudi kujitafutia nguvu mpya na bora katika ushirikiano na ushindani wa kiuchumi wa kimataifa. Nguvu za nchi zinazoendelea zitaongezeka, hivyo pengo la nguvu kati ya nchi mbalimbali litapungua. Sisi tunatetea zaidi kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, yaani mbali na kujitafuta maslahi, pia ni lazima kuzingatia maslahi ya nchi nyingine. Nchi mbalimbali zinapaswa kusaidiana na kubeba majukumu kwa pamoja ili kuhimiza utaratibu wa kimataifa uendelee kwa mwelekeo wa haki na halali zaidi. "

    Kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, Bw. Yang Jiechi amesema historia ya miaka 40 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi imeonesha kuwa, maafikiano yananufaisha pande hizo mbili, na mapambano yanaleta madhara kwa pande mbili. China na Marekani zinapaswa kufuata taarifa tatu za pamoja na kanuni za taarifa ya pamoja kati ya nchi hizo mbili, na kila upande unatakiwa kuheshimu maslahi makuu na ufuatiliaji mkubwa wa upande mwingine.

    Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika kwa saa mbili, Bw. Yang Jiechi pia ameeleza misimamo ya China katika uhusiano kati ya China na Russia, na India, na Japan, suala la peninsuala ya Korea, suala la Libya na uhusiano kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako