• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa biashara wa China akana lawama za Marekani kuhusu China kutofuata kanuni za WTO

    (GMT+08:00) 2012-03-07 18:13:20

    Hivi karibuni Marekani iliilaani China kuwa haifuati kanuni za Shirika la Biashara la Dunia WTO, na lawama zake hasa ni dhidi ya utoaji ruzuku wa China. Waziri wa biashara wa China Bw. Chen Deming amesema China siku zote inafuata kanuni za WTO, na kwamba serikali kuu ya China haitoi ruzuku zinazopigwa marufuku na WTO, na kama imetoa ruzuku kwa sehemu fulani, China inapenda kujadili jambo hili.

    Alipokutana na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa 5 wa bunge la umma la China, Bw. Chen amesema, toka ijiunge na WTO miaka 11 iliyopita, China siku zote inafuata kanuni za WTO, lakini haipaswi kuwajibika kutekeleza sheria na kanuni za nchi fulani ambazo haziendani na kanuni za mashirika ya kimataifa.

    Tarehe 6 Machi baraza la chini la bunge la Marekani lilipitisha sheria ya ushuru likitoa idhini kwa wizara ya biashara ya Marekani kuendelea kutoza ushuru wa kupinga ruzuku kwa nchi zisizo na uchumi wa soko huria zikiwemo China na Vietnam. Sheria nyingine inayofanana na hiyo ilipitishwa tarehe 5 kwenye baraza la juu la bunge la Marekani.

    Bw. Chen Deming amesema wizara ya biashara ya Marekani haijasahihisha makosa yake, na kitendo chake kimekwenda kinyume na kanuni za kimataifa na sheria za Marekani.

    Akizungumzia suala la ruzuku, Bw. Chen amesema Shirika la Biashara la Dunia limebainisha ruzuku ya kupigwa marufuku na ruzuku inayotokana na hali Fulani. Nchi wanachama wengi wa WTO zinatoa ruzuku mbalimbali, na zina tafsiri zao tofauti kuhusu ruzuku hizo.

    Amesema China inapenda kufanya mazungumzo na nchi zinazoilaumu, ili kujadili ruzuku zinazotolewa kwa sehemu fulani. Pia amesema wazi kuwa serikali kuu ya China haitoi ruzuku zilizopigwa marufuku.

    Tarehe 28 Februari, Rais Barack Obama alisaini waraka unaoruhusu kuunda kituo cha utekelezaji wa sheria za biashara, ili kuchukua hatua dhidi ya nchi ambazo huenda zitadhuru makampuni ya Marekani.

    Bw. Chen Deming amesema uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni msingi muhimu wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili na nguvu kubwa ya kuhimiza maendeleo ya uhusiano huo. China itafuatilia kwa karibu kituo hiki cha Marekani, na italinda maslahi halali ya makampuni ya China kwa mujibu wa sheria, na kuwasiliana na kituo hiki kwa kutumia kanuni za biashara za kimataifa ili kulinda maslahi ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako