• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchagua wajumbe wa bunge la umma wa mijini na vijijini kwa uwiano sawa

    (GMT+08:00) 2012-03-08 17:58:29

    Mwaka kesho China itachagua wajumbe wa bunge la umma kwa kigezo sawa cha idadi ya watu mijini na vijijini, hii itawezekana kama rasimu ya uamuzi wa uchaguzi wa wajumbe iliyowasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura itapitishwa. Kwa mara ya kwanza idadi ya wajumbe 2000 wa bunge la 12 la umma itatolewa kwa maeneo ya mijini na ya vijijini kwa uwiano sawa. Uchaguzi wa wabunge wa bunge la 12 la umma utakamilika mwezi Januari mwaka kesho, miezi miwili kabla ya kwisha kwa kipindi cha bunge la 11 la umma.

    Naibu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la China Bw Li Jianguo amesema wajumbe wa bunge la umma ni sehemu muhimu ya nguzo muhimu ya dola wanaowakilisha maslahi na matakwa ya watu, na wanashiriki katika kutunga sheria na kutumia madaraka ya dola. Sehemu muhimu ya uchaguzi unaokuja ni kuwachagua wajumbe kwa mujibu wa uwiano sawa wa idadi ya watu mijini na vijijini.

    Bw Li pia amesema mafanikio ya uchaguzi huo yatakuwa na umuhimu mkubwa katika kuendeleza siasa za ujamaa zenye demokrasia, kuhakikisha kuwa watu ndio waamuzi wa mambo ya nchi, na katika kujenga nguvu ya dola. Pia yatasaidia kukusanya pamoja busara na nguvu kutoka sekta mbalimbali, kuhimiza maendeleo kwa njia ya kisayansi na kuimarisha masikilizano katika jamii.

    Rasimu ya uamuzi kuhusu uchaguzi imeandaliwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyofanyiwa mabadiliko kwa lengo la kuleta usawa kwa wananchi wote, mikoa yote na makabila yote. Bw Li amefafanua kuwa kila watu laki 6.7, wa mijini au vijijini watawakilishwa na mjumbe mmoja wa bunge la umma.

    Mikoa 31, mikoa inayojiendesha na manispaa zote za China bara, bila kujali ukubwa wake, zitapewa misingi sawa wa idadi ya wajumbe. Rasimu ya katiba inasema kila mkoa utapewa idadi ya msingi ya wajumbe 8, na kufanya jumla ya idadi kuwa 248. Baadhi ya nafasi za wajumbe zitatengwa kwa ajili ya kamati ya kudumu ya bunge la umma, ili kuhakikisha kuwa kila kabila, bila kujali ni dogo kwa kiasi gani linaweza kuwa na mjumbe walau mmoja wa bunge la umma.

    Wachambuzi wa mambo ya sheria wameisifu rasimu hiyo mpya ya katiba wakisema inatoa haki sawa za kuchagua wajumbe kwa watu wa mijini na vijijini, inahimiza demokrasia na uwakilishi katika mfumo wa bunge la umma la China. Mkuu wa Idara ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Umma Bw Ha Dayuan amesema, kutokana na idadi kuwa ya watu kuhamia mijini, ukuaji wa miji umeongezeka Pengo la maendeleo kati ya mikoa na kati ya miji na vijiji linapungua, hii imeweka mazingira mazuri ya kuwepo kwa haki sawa ya kuchagua wajumbe wa bunge la umma la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako