• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la umma la China lathibitisha mswada wa marekebisho ya sheria kuhusu mashtaka ya uhalifu wa kijinai

    (GMT+08:00) 2012-03-08 19:12:34

    Mkutano wa 5 wa Bunge la 11 la umma la China leo tarehe 8 umeitisha mkutano wake wa pili wa wajumbe wote, ambapo wamesikiliza ripoti na kujadili mswada wa marekebisho ya sheria kuhusu mashtaka ya uhalifu wa kijinai. Mswada huo umeongeza kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" kwenye sheria hiyo, hii imeonesha kanuni muhimu ya katiba kuhusu kuhakikisha haki ya binadamu.

    Naibu spika wa bunge la umma Bw. Wang Zhaoguo siku hiyo alipotoa ufafanuzi kuhusu mswada huo alisema, kuongeza kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" kwenye sheria hiyo kunatokana na kwamba utaratibu wa mashitaka ya uhalifu wa kijinai unahusiana na uhuru wa raia na haki nyingine za kimsingi, kufanya hivyo kunasaidia kuonesha ipasavyo utaratibu wa kijamaa wa sheria za China, pia kunasaidia kufuata vizuri zaidi kanuni za katiba kuhusu kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu wakati wa kushughulikia kesi za uhalifu wa kijinai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako