• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" chawekwa kwenye sheria ya mashtaka ya uhalifu wa jinai

    (GMT+08:00) 2012-03-09 18:22:14

    Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Bunge la umma la China unaofanyika sasa hapa Beijing, wameanza kujadili mswada wa marekebisho ya "Sheria ya mashtaka ya uhalifu wa jinai". Kwenye mswada huo, kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" kimeongezwa, na kinahusisha vipengele mbalimbali vya uandikishaji mashtaka, uchunguzi, kusikiliza kesi na kutoa hukumu. Wajumbe na wataalamu kuhusu haki za binadamu wanaona kuwa, marekebisho ya sheria hiyo yameonesha kuwa, mfumo wa sheria wa China unapata maendeleo makubwa siku hadi siku, na ni hatua kubwa katika mambo ya haki za binadamu nchini China.

    Haya ni marekebisho ya pili kufanyika katika sheria ya mashtaka ya uhalifu wa jinai tangu sheria hiyo itungwe mwaka 1979. Katika marekebisho mapya, vifungu 65 vimeongezwa, sehemu 110 za vifungu vya sheria hiyo zimerekebishwa, na marekebisho makubwa zaidi kwenye sheria hiyo ni kuwekwa kwa kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu". kifungu hichi kinaweka bayana kuwa, ni marufuku kumlazimisha mtu yeyote kukiri kufanya uhalifu; kulinda haki ya kujitetea ya watuhumiwa; kulinda raia kutokamatwa bila kufuata sheria, na kuhakikisha uhuru wa raia. Akijadili mswada huo, mjumbe wa bunge la umma Bw. Wang Liming amesema, kuwekwa kwa kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu" kwenye sheria ya mashtaka ya uhalifu wa jinai ni maendeleo makubwa yaliyopatikana katika mambo ya haki za binadamu nchini China. Anasema:

    "Naona marekebisho ya sheria hiyo yanayonivutia zaidi ni kuhusu kuwekwa kwa kifungu cha "kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu", hayo ni maendeleo makubwa yanayostahiki kusifiwa."

    Lakini China ni nchi kubwa inayoendelea, na idadi ya watu wake imefikia bilioni 1.3. Kutokana na maendeleo yasiyo ya uwiano katika sehemu mbalimbali nchini China, hali ya haki za binadamu bado inakabiliwa na changamoto nyingi. Kama alivyosema makamu wa rais wa China Xi Jinping wakati alipotembelea Marekani mwezi uliopita, kwamba hakuna hali ya haki za binadamu isiyo na dosari, lakini watu wanaweza kuifanya hali hiyo iwe nzuri zaidi. Kwa kufuata hali halisi ya nchi, serikali ya China itaendelea kutoa kipaumbele katika ufuatiliaji wa maslahi ya watu, kuzingatia kwa makini matumaini na matakwa ya wananchi katika masuala yote, na kuchukua sera na hatua halisi kwa ajili kuhimiza usawa, haki na masikilizano kwenye jamii, ili, siku hadi siku, maendeleo mapya yapatikane katika mambo ya haki za binadamu nchini China.

    Naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa haki za binadamu katika Taasisi ya sayansi ya jamii Bw. Liu Huawen anasema:

    "Kuna kanuni moja katika sheria ya kimataifa, yaani mambo ya haki za binadamu yanapaswa kuendelea, na si kurudi nyuma, ni lazima kufanya juhudi zisizolegea katika kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu, kufanya hivyo kunatakiwa kuwa na nia ya kisiasa, pia kuwa na uhakikisho wa utaratibu. Kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu ni matumaini wanayotafuta watu wa dunia nzima, bado kuna mambo mengi tunayopaswa kufanya ili kufikia matumini hayo, hayo ni mambo yanayotaka watu wote washikilie na kujitahidi bila kusita."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako