• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumaini ya Mzee Maimaitijiang

    (GMT+08:00) 2012-10-29 19:54:46

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China utafanyika hivi karibuni, ambapo wajumbe wapatao zaidi ya 2200 watakusanyika Beijing kujadili na kuamua masuala mengi mbalimbali yanayohusu mustakbali wa chama tawala na yatakayoleta athari kubwa kwa China katika siku za baadaye. Sasa tunawaletea ripoti kuhusu matarajio ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.

    Wasikilizaji wapendwa, mnaosikia ni wimbo uliosikika katika kijiji cha kabila la wahui mkoani Hubei, Bw. Wei Dengdian anayetajwa kwenye wimbo huu ni katibu wa chama wa kijiji hicho. Bw. Wei alirudi katika kijiji chake cha Kanzi mwaka 1975 baada ya kujiunga na jeshi, umri wake unakaribia miaka 60 sasa, mzee huyo siku zote anashikilia matumaini yake, kuwa ni lazima kuwawezesha wanakijiji wenzake waishi maisha mazuri. Akisema:

    "Naona ni lazima kuwa na watu wanaoweza kutangulia mbele ili kuwahamasisha wakazi wa kijiji cha Kanzi kufanya juhudi za kuendeleza uzalishaji na kupata maisha mazuri. Hili ni lengo langu la mwisho, hivyo siwezi kuondoka katika maskani yangu Kanzishan, napenda kutoa mchango wangu kwa ajili ya ujenzi wake."

    Kijiji cha Kanzi aliko Bw. Wei Dengdian ni kijiji kilichoko mbali zaidi mkoani Hubei, inachukua muda wa saa nne kwa gari kutoka mji wa wilaya hadi kwenye kijiji hicho. Katika miaka 37 iliyopita, Bw. Wei amewaongoza wanakijiji wa kabila la wahui na wahan kujenga kijiji chao kilichokuwa maskini, kuwa kijiji kipya chenye barabara, kutumia umeme, maji ya bomba, simu na televisheni. Mwezi Juni mwaka huu Bw. Wei alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa 18 wa chama cha kikomunisti cha China, amesema kwenye mkutano huo atatekeleza jukumu lake akiwa mjumbe wa umma wa watu wa makabila madogo katika sehemu ya mbali mlimani, na atatoa maoni na matarajio ya wakazi wa huko kwenye mkutano mkuu wa chama.

    Mkurugenzi wa Kijiji Brukai mkoani Xinjiang Bw. Maimaitijia Wumaier pia ni mtangulizi aliyeongoza wanakijiji wenzake kujiendeleza. Katika kijiji chake Brukai wanaishi watu wa makabila ya wauyghur, wakhazak na wahan. Bw. Maimaitijiang anasema, ni muhimu zaidi kuwawezesha wanakijiji wa makabila mbalimbali wawe na mshikamano, ili kuhimiza maendeleo ya kijiji chao. Akisema:

    "kama hakuna mshikamano wa watu wa makabila mbalimbali hakutakuwa na utulivu wa jamii, kama hakuna utulivu jamii, basi hatutaweza kupata maendeleo, na sisi raia hatutaweza kupata maisha mazuri."

    Bw. Maimaitijiang aliwaongoza wanakijiji wenzake kwenda katika sehemu nyingine kujifunza ufundi na uzoefu wa wengine, kuingiza mbegu bora kutoka nje, huku akienda katika idara za serikali kuomba msaada wa kisera, kutafuta miradi mipya, na kuendeleza shughuli za ufugaji. Hivi sasa kijiji Burikai kimekuwa na mashamba ya vielelezo vya kilimo cha ngano, bustani ya miti ya matufaha, na kituo cha ufugaji kwa kufuta vigezo, ambapo mabadiliko makubwa yametokea katika maisha ya wanakijiji, mapato ya kila mwanakijiji yamezidi yuan elfu 8 kwa mwaka. Bw. Maimaitijiang amechaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa 18 wa chama, amesema, amefanya juhudi anazostahili kuzifanya, na atajitahidi kufanya vizuri zaidi kwa ajili ya kijiji chake.

    Na Bibi Hong Hanying mwenye umri wa miaka 47 ni mtu wa kabila la washibo mkoani Xinjiang, anafanya kazi katika chuo kikuu cha matibabu na a za ya Kichina cha Shanghai. Kwa kuwa anaelewa zaidi utamaduni, mila na desturi za makabila madogomadogo na sera husika za makabila, pia anajua lugha za makabila kadha wa kadha, hivyo anapewa kazi ya kuwasaidia wanafunzi kutoka makabila madogomadogo. Kila ifikapo mwezi Septemba wakati chuo kinapofunguliwa, huwa anawakusanya wanafunzi kutoka makabila madogomadogo kuwasaidia kushinda taabu za maisha na masomo, amesifiwa sana na wanafunzi. Lakini yeye mwenyewe anaona kuwa bado hajafanya kazi kubwa, lakini anawasaidia wanafunzi kwa moyo dhati ili wawe watulivu katika maisha na masomo na kutimiza matarajio yao ya siku za baadaye.

    Miongoni mwa wajumbe watakaohudhuria mkutano mkuu wa 18 wa chama cha kikomunisti cha China, kuna wajumbe wengi kama Bw. Wei Dengdian, Maimaitijiang na Hong Hanying, ambao wanafanya kazi za kawaida, lakini wametoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako