• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zanufaishwa na maendeleo ya China

    (GMT+08:00) 2012-11-09 18:43:42

    Swali: Profesa kwamba tarehe nane mwezi ujao (Novemba 8) chama cha kikomunisti cha uchina kinachagua viongozi wake. Unpoangalia ushirikiano wa Kenya na China miaka kumi iliyopita, je unaweza kusema nini?

    Jibu: Naam, kwa miaka kumi iliyopita, taifa la China limeweza kuchangia kubwa sana hasa katika upande wa miundo mbinu ya taifa la Kenya. Na ukiangalia barabara nyingi zajengwa na wachina na pia hata baadhi ya vifaa ambavyo tunavitumia huko vinatoka uchina, biashara imeweza kufungukwa kwa ukubwa sana. Wafanyabiashara wa Kenya wameweza kutoa vitu vingi kutoka China, wanaweza kunufaishwa na vifaa hivyo. Tunaona ni kwamba, baada ya uchaguzi ujao, uhusiano baina ya Kenya na China utaendelea kuimarika na utaendelea kushika nguvu zaidi na kwa sababu nchini Kenya kumegundulika pia na maliasili nyingi. Kumegundulika mafuta, kumegundulika pia na gesi na hata makaa na dhahabu na vitu kama hivyo, na ukiangalia namna ambavyo taifa la China limeweza kuwekeza katika maliasili kusini mwa Afrika, Botswana hata na DRC inaonekana moja kwa moja kwamba watakapochagua kiongozi mpya na yeye pia ataendeleza uhusiano huu katika mataifa ya Afrika ya Mashariki ambayo kwa sasa kwa mara ya kwanza yameonekana yana raslimali nyingi sana. Kwa hivyo mimi nahisi kwamba ushirikiano utaendelea kuimarika hautabadilika utakita mizizi zaidi na huenda hata kuwa na mashindano baina ya China na mataifa ya magharibi ambayo yameona manufaa ya kuwa na uhusiano na mataifa ya Afrika.

    Swali: Hivyo umezungumzia kuhusu miundo mbinu ambayo China imewekeza Kenya na Afrika kwa ujumla, inapokuja kwa mtu wa kawaida, je amenufaika vipi?

    Jibu: Naam, unajua kwamba ikiwa unataka kuimarisha taifa, mahala pa kuanzia kabisa huwa ni miundombinu. Ikiwa kuna barabara nzuri, basi yule mtu wa kawaida anaweza kusafisha bidhaa zake kutoka mahala anapozalisha bidhaa hizo, na kuzipeleka mahala kwingine. Kwa hivyo, bila shaka tunaweza kusema kwamba mwananchi wa kawaida ananufaishwa na barabara ambazo zinajengwa na Wachina. Jambo jingine ambalo linamnufaisha mwananchi wa kawaida ni kwamba bidhaa za China baadhi yake, bei yake iko chini ukilinganisha na za bidhaa kutoka mataifa ya nje, na kwa hivyo mwanachini wa kawaida ambaye hapo nyuma hangeweza kuwa na mavazi mazuri, ama hangeweza kuwa labda na vifaa vya umeme na vifaa kama hivyo, ambavyo vinapatikana kwa vyepesi zaidi China, mwananchi huyu anapata nafasi ya kuvipata kwa vyepesi zaidi na kwa bei ambayo ni fuu. Changamoto tu ni kwamba itaibidi serikali ya China yaanze sasa kumnufaisha mwananchi wa kawaida kwa kufungua milango yake kwa mfanyabiashara mdogo katika taifa la China, yaani ile kwmaba isiyo kwamba biashara hii ni ya mkondo mmoja iwe ni ya mikondo yote miwili, biashara vifaa vya kutoka Kenya viweze kupata soko lake katika taifa la China, na hali kadhalika na siye pia tuweze kupata bidhaa kutoka China. Hali kadhalika kuna vitu vingine ambavyo nafikiri ni muhimu pia kuweza kuvifikiria, ni labda elimu kwa mwananchi wa kawaida, milango iweze kufunguliwa kwa kuweza kumwezesha Mkenya aweze kunufaishwa hasa na elimu ya kiteknolojia ambayo inapatikana kwa Uchina kwa kiwango kikubwa, na ikiweza kufanika hivyo, basi tutakuwa na ushirikiano wa karibu zaidi, binafsi nahisi kwamba matumaini kwa mataifa ya Afrika hayako katika uhusiano wa mataifa ya Afrika na mataifa ya magharibi, matumaini ya Afrika yako katika uhusiano baina ya Afrika na mataifa ya Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako