• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashikilia "ushirikiano na maendeleo kwa pamoja" katika mambo ya kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2012-11-13 18:26:33

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China leo unaendelea hapa Beijing. Katika ripoti iliyotolewa na kuthibitishwa kwenye mkutano huo, chama tawala kimefafanua sera zake za mambo ya ndani na nje.

    Ripoti hiyo imeeleza wazi kuwa, China itajitahidi kuyafanya maendeleo yake yanuzifaishe zaidi nchi jirani. Mtafiti wa Idara ya utafiti ya mambo ya kimataifa na mikakati Bw. Gao Zugui anaona kuwa, msimamo huu wa China unaambatana na sera ya siku zote inayofuata China ya "kutendeana vizuri na majirani na kuzichukulia nchi jirani kuwa marafiki". Akisema:

    "Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya China katika mambo ya uchumi na jamii, sehemu zilizoko pembezoni mwa China hata dunia nzima zinataka kupata manufaa kutokana na maendeleo ya China. Hatua zijazo ni namna sisi tutakavyojitahidi zaidi kuzifanya nchi jirani na hata dunia nzima inufaike."

    Katika siku za karibuni migogoro kuhusu mamlaka ya ardhi na bahari kati ya China na nchi husika za jirani imekuwa inafuatiliwa zaidi. Mkurugenzi wa Tawi la Beijing la Kituo cha Televisheni ya Japan TBS Bw. Inoue Yoichi amemwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, aliposikiliza ripoti iliyotolewa na katibu mkuu wa chama tawala cha China Hu Jintao aliguswa zaidi na maelezo yake kuhusu China italinda kithabiti haki na maslahi ya nchi katika mambo ya bahari. Na naibu mkuu wa Chuo kikuu cha mambo ya kidiplomasia cha China Bw. Qin Yaqing akisema:

    "Katika ripoti hiyo China imesisitiza kulinda haki na maslahi katika mambo ya bahari, hii ni muhimu sana. Nchi yoyote yenye mamlaka inapaswa kufanya hivyo. Lakini ripoti hiyo imesisitiza kuwa mikakati yetu ya ulinzi ni ya kujihami. China inashikilia msimamo wake wa kufanya majadiliano na mazungumzo kutatua tatizo la ardhi, huu ni msimamo wa kimsingi wa kikanuni, naona serikali ya China siku zote haitabadilisha msimamo huo."

    Ripoti hiyo pia imefafanua wazi kuwa, China itaendelea kuinua bendera ya amani, maendeleo, ushirikiano na maendeleo kwa pamoja", juu ya hiyo Bw. Qin Yaqing akisema:

    "Katika mchakato wa amani na maendeleo, ni lazima tufanye ushirikiano ili kupata maendeleo kwa pamoja, yaani pande mbili zote zinufaike, na zote zioneshe nia yake ya kufanya ushirikiano. Kama watu wakidhani China itatumia nguvu yake inayotokana na maendeleo, na kutumia mbinu za mabavu kutafuta maslahi yake, basi watu hao hawajaelewa utawala wa China, mikakati mikubwa ya China pamoja na njia iliyopita China katika miaka 30 iliyopita."

    Kuhusu maendeleo ya baadaye kati ya China na nchi kubwa, ripoti hiyo kwenye mkutano mkuu imefafanua kuwa, China itahimiza kujenga uhusiano mzuri wa aina mpya ulio wa kudumu na utulivu kati yake na nchi kubwa. Kwa mfano wa uhusiano kati ya China na Marekani, marais wa nchi hizi mbili walikutana mara 26 katika miaka 10 iliyopita, na taratibu zaidi ya 90 kati ya serikali, ukiwemo utaratibu wa mazungumzo ya mikakati na uchumi kati ya China na Marekani zimeanzishwa. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Yang Jiechi alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani katika siku za baadaye alisema, pande mbili zinapaswa kutupia macho zaidi maslahi ya kimsingi ya wananchi wa nchi hizo mbili na maslahi ya pamoja ya watu wa dunia nzima, ili kusukuma mbele siku hadi siku maendeleo ya uhusiano huo.

    Na Bw. Qin Yaqing akitafsiri anasema, kujenga uhusiano wa aina mpya kati ya nchi kubwa kunazitaka nchi zote kubwa zifuate njia ya amani na kufanya mazungumzo ili kutatua matatizo. Kwa upande mmoja nchi kubwa zinapaswa kushirikiana ili kufanya mambo mengi zaidi kwa ajili ya binadamu, na kwa upande mwingine zinatakiwa kuondoa migogoro na migongano kati yao kwa njia sahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako