• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Kenya asema Chama cha Kikomunisti cha China kina uwezo mkubwa wa kuitawala China

    (GMT+08:00) 2012-11-14 16:02:13

    Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema kuwa, anaamini Chama cha Kikomunisti cha China kina uwezo mkubwa katika kuitawala vizuri nchi ya China. Odinga amesema hayo alipohojiwa na mwandishi wa Habari wa CRI mjini Nairobi. Amesema, "Siwezi kusahau jinsi China inavyobadilisha awamu mpya ya viongozi wao, madaraka ya uongozi yanakabidhiana kwa njia nzuri. Mchakato wa uchaguzi umeonesha maoni ya wananchi kuanzia vijijini hadi kamati kuu ya chama. Bila shaka mfumo huo mzuri wa uongozi una uwezo wa kushughulikia vizuri mambo ya China, ambayo ni nchi kubwa yenye watu wengi zaidi duniani. Natumaini kwamba mipango mbalimbali itatungwa katika mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China, ikiwemo mipango inayohusu kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika. Kwa sasa China iko katika kipindi muhimu sana, naitakia China pamoja na wananchi wake mafanikio makubwa katika siku za baadaye."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako