• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi lathibitishwa kuwa fikra ya uelekezaji kwenye Katiba ya chama

    (GMT+08:00) 2012-11-14 17:56:31

    Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China umefungwa leo tarehe 14 hapa Beijing. Chama cha Kikomunisti cha China imefanya marekebisho ya 18 ya katiba yake ambayo ni mwongozo wa utawala wa nchi, ambapo wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi limethibitishwa kuwa fikra ya uelekezaji wa chama pamoja na Umarx-lenin, Fikra ya Mao Zedong, Nadharia ya Deng Xiaoping na "Uwakilishi mtatu".

    Kiini cha wazo kuhusu kujiendeleza kwa njia ya kisayansi ni kutoa kipaumbele kwa maslahi ya watu. Kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi, China yenye idadi kubwa zaidi ya watu imetatua kimsingi suala la chakula kwa watu wake. Mwandishi wetu wa habari alipowahoji wachina wa kawaida ameona kuwa, watu wengi wanafuatilia zaidi masuala kuhusu namna ya kuongeza mapato yao, kuwa na hewa safi zaidi, maji safi zaidi, na mazingira mazuri zaidi.

    Aidha, wachina wengi wamekuwa na mahitaji zaidi ya kiroho. Kwa mfano, mama kichanga Xu Ruo anafuatilia zaidi kama utaratibu wa elimu utakamilika zaidi au la, ili mtoto wake aweze kukua kwa furaha zaidi. Akisema:

    "Wazazi wengi wa watoto wanatarajia mageuzi yafanyike katika mambo ya elimu. Kwani utaratibu wetu wa elimu unawafanya watoto wetu watingwe na masomo na kukabiliana na mitihani mingi, kutokuwa na fursa ya kufurahia utoto wao na kupoteza uwezo wa kufanya uvumbuzi na nia ya kushirikiana na wenzao. Ni lazima kutilia mkazo elimu juu ya sifa za watoto, na kuwawezesha wawe na moyo wa kufanya ushirikiano na wengine".

    Matumaini na matarajio ya wachina yameonesha mabadiliko ya zama tulizonazo. Katika kipindi kipya cha zama mpya, Chama cha Kikomunisti cha China kimeliweka wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi kuwa fikra ya uelekezaji wa chama katika katiba. Kwa maoni ya msomi wa China Bw. Cai Zhiqiang, marekebisho hayo ya katiba yameonesha uvumbuzi mpya wa nadharia muhimu ya chama, zaidi yameonesha mkakati muhimu wa chama wa kuwaongoza wananchi kusonga mbele katika njia ya kujenga jamii yenye maisha bora kote nchini, hili ni jibu la chama kwa matarajio ya wananchi juu ya maisha bora. Bw. Cai anasema:

    "Sera za chama kuweza kukidhi mahitaji ya watu wa makundi tofauti au la, kunahusiana zaidi na maslahi ya wananchi wengi, wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi kihalisi ni lengo la kimsingi la chama tawala, vilevile ni matarajio mapya kwa maisha ya wananchi."

    Mtaalamu maarufu wa Hispania kuhusu masuala ya China Bw. Julio Rios alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema:

    "Katika misamiati ya kawaida ya siasa, wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, maana yake ni kama "maendeleo endelevu", lakini wazo hilo linahusisha mambo mengi zaidi kuhusu maendeleo endelevu. Kwani maendeleo endelevu huwa yanamaanisha kuhifadhi mazingira wakati wa kuendeleza uchumi, lakini wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi linamaanisha kuratibu kwa uwiano pande mbalimbali za maendeleo ya jamii. Wakati wa kujiendeleza ni lazima kutilia mkazo sifa ya kazi, ni lazima kuwanufaisha wananchi wote, si kama tu kuwanufaisha wananchi wa China, bali pia kwa kanda hata dunia nzima."

    Katika mswada wa marekebisho ya katiba ya Chama cha kikomunisti cha China, kazi ya kujenga ustaarabu wa kuhifadhi mazingira ya viumbe kwa mara ya kwanza imewekwa kwenye katiba ya chama, na ufafanuzi wake umesema, Chama cha Kikomunisti cha China kitashikilia kufuata njia ya kujiendeleza kwa ustaarabu katika kuendeleza uzalishaji, kuboresha maisha ya watu na kujenga mazingira mazuri ya viumbe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako