• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano mkuu wa 18 wa CPC wamalizika

    (GMT+08:00) 2012-11-14 19:03:17

    Mkutano mkuu wa 18 wa chama cha kikomunisti cha China umefungwa leo tarehe 14 hapa Beijing. Mkutano huo umetoa wito kwa wanachama wote wasonge mbele bila kusita kufuata njia ya ujamaa wenye umaalum wa China, na kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora kote nchini.

    Ripoti iliyotolewa kwenye mkutano huo na katibu mkuu wa chama hicho Hu Jintao, imesisitiza tena malengo makubwa mawili ya China katika miongo kadhaa ijayo, yaani ifikapo mwaka 2049, wakati wa maadhimisho ya miaka 100 ya Jamhuri ya Watu wa China, jamii yenye maisha bora kote nchini itakuwa imejengwa, na nchi ya kisasa ya ujamaa yenye nguvu, usitawi na neema, demokrasia, ustaarabu na hali ya masilikizano itakuwa imejengwa.

    Mkutano huo umechangua wajumbe wa kamati kuu mpya ya chama, wajumbe wa kamati kuu mpya ya ukaguzi wa nidhabu, na kupitisha ripoti iliyotolewa na kamati kuu ya 17 ya Chama cha kikomunisti cha China, ripoti ya kazi ya kamati kuu ya ukaguzi wa nidhamu, na rasimu ya marekebisho ya Katiba ya Chama cha kikomunisti cha China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako