• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya kisasa ya mali za urithi za utamaduni mjini Xi'an

    (GMT+08:00) 2013-07-01 16:17:15

    Baadhi ya watu wanaona kuwa historia ya mji mmoja ni historia ya kabila moja. Mji wa Xi'an wa mkoa wa Shaanxi ulioko magharibi mwa China ulikuwa mji mkuu wa enzi 13 za China, na hivi sasa mji huo unajulikana kama ni mmoja kati ya miji minne mikubwa ya ustaarabu wa binadamu, pamoja na miji ya Athens, Cairo na Rome. Mji huo pia ni kituo cha kwanza cha "Njia ya Hariri" ambayo ni njia ya kibiashara inayounganisha mabara ya Asia, Afrika na Ulaya. Hivi sasa kwa kutegemea mambo ya utamaduni mkubwa, mji huo wenye historia ndefu sasa una unastawi mpya.

    Mji wa Xi'an una vivutio vingi vya kitalii. Kuanzia miaka zaidi ya 2,000 iliyopita wakati mfalme Qinshihuang alipoanzisha nchi ya kwanza ya China iliyounganishwa, enzi 13 ziliufanya mji huo kuwa mji mkuu wao. Mabaki ya vitu na utamaduni wenye historia ndefu yameufanya mji huo ujulikane kama jumba kubwa la makumbusho ya historia. Mkoani Shaanxi kuna sehemu muhimu zaidi ya 600 za hifadhi ya mabaki ya historia. Kati ya sehemu hizo, ile yenye sanamu za askari na farasi za kaburi la mfalme Qinshihuang iliyoko umbali wa kilomita kadha kutoka mji wa Xi'an inajulikana kama "Muujiza mkubwa wa nane duniani".

    Shughuli ya utalii ni nguzo ya uchumi wa mji wa Xi'an. Ukiwa mji wa kitalii, Xi'an una mtandao bora wa barabara. Kote mjini humo, kuna barabara zaidi ya 40 zinazoelekea kwenye sehemu zenye vivutio vya utalii kutoka kwa sehemu ya katikati ya mji, na barabara maalumu zaidi ya 10 za kitalii. Mji wa Xi'an pia ni mji wa kwanza wenye subway kati ya miji ya kaskazini magharibi mwa China. Mbali na hayo, mji huo una taksi zaidi ya elfu 10.

    Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli ya utalii zinaendelezwa kwa kasi katika mji huo. Haswa baada ya kuzinduliwa kwa reli ya treni ya kasi kubwa inayounganisha mji wa Xi'an na miji mikubwa ikiwemo Beijing, Shanghai, Guangzhou na Wuhan, muda wa kusafiri kati ya mji wa Xi'an na miji hiyo umepungua kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano umbali kati ya miji ya Xi'an na Beijing ni kilomita zaidi ya 1,200, lakini ukisafiri kwa treni ya aina hilo, itakuchukua muda wa zaidi ya saa nne tu. Takiwmu zinaonesha kuwa mwaka 2012, idadi ya watu kutoka nchi za nje waliotalii mjini Xi'an ilifikia milioni moja. Bibi Mu Yanxi ni mfanyakazi wa shirika la utalii la Xibeiguoji mjini Xi'an. Alisema,

    "Ninafanya kazi katika kituo cha treni ya kasi. Kazi yangu ni kuwapokea watalii wanaokuja hapa China kwa treni. Watalii hao wanatoka sehemu mbalimbali nchini China na nchi za nje."

    Mji wa Xi'an una vitu vingi vya mabaki ya utamaduni ya zama za kale vyenye thamani kubwa, pia una vitu vingi visivyoonekana vya utamaduni wa historia. Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo umefanya juhudi kubwa ili kutafuta thamani ya kisasa ya mali za urithi za utamaduni. Mtaa wa utamaduni wa zama za kale wa Shuyuanmen ni mfano mzuri wa utekelezaji wa juhudi hizo. Watalii wanaofika mji wa Xi'an si kama tu wanapaswa kutembelea sanamu za askari na farasi za kaburi la mfalme Qinshihuang na jumba la makumbusho ya historia la mkoa wa Shaanxi, bali pia wanapaswa kutembelea mtaa huo wenye kivutio kikubwa cha utamaduni.

    Mtaa wa utamaduni wa zama za kale wa Shuyuanmen uko karibu na jumba maarufu la makumbusho ya minara la mji wa Xi'an. Mbele ya mtaa huo kuna mlango mkubwa wenye mtindo wa kichina wa zama za kale. Katika mtaa huo majengo yote ni ya mtindo wa zama za kale, na barabara zote zilijengwa kwa kutumia mawe ya asili badala ya saruji ya kisasa. Mtaa huo una historia ndefu. Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, kwa mujibu wa mpango wa marekebisho ya mji wa Xi'an, mtaa huo ulikarabatiwa na kuwa mtaa wa kibiashara kwa kuiga mtindo wa enzi za Ming na Qing. Hivi sasa katika mtaa huo kuna maduka mengi ya picha za uchoraji na maandishi, na zana za uchoraji. Katika mtaa huo, licha ya kununua vitu hivyo, watalii pia wanaweza kuchora picha wao wenywe. Mwenye duka mmoja wa mtaa huo alisema,

    "Hapa ni sehemu yenye mambo mengi zaidi ya utamaduni na historia. Tunauza picha, karatasi, kalamu na chai. Shughuli zetu pia ni za kiutamaduni."

    Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya mji wa Xi'an imekuwa inatilia maanani sana kujenga na kuendeleza mitaa ya kibiashara yenye vivutio maalumu, na kuunga mkono maendeleo ya mitaa hiyo kwa juhudi za kutunga mipango, kutekeleza sera za kipaumbele, na kutoa msaada wa fedha. Hivi sasa mji huo una mitaa ya aina hiyo zaidi ya 40.

    Wakati serikali ya mji wa Xi'an inapojitahidi kulinda mabaki ya historia, pia inatilia maanani kuchanganya mali za urithi za utamaduni na maisha ya wakazi. Ujenzi wa bustani ya mabaki ya ukuta wa ulinzi wakati wa enzi wa Tang unaweza kuonesha mawazo hayo. Ili kulinda ukuta huo wenye urefu wa kilomita 3.7 uliojengwa miaka 1,300 iliyopita, mji wa Xi'an uliwekeza karibu renmibi yuan milioni 500, ili kufanya ukarabati na kuweka alama ya uhifadi katika sehemu mbalimbali za ukuta huo na mto wa ulinzi ulioko nje ya ukuta huo. Mbali na hayo katika bustani hiyo, miji na nyasi nyingi zimepandwa ili kuboresha mazingira. Hivi sasa bustani hiyo si kama tu inawavutia watalii kutoka sehemu mbalimbali, bali pia ni sehemu nzuri ya wakazi wa mji wa Xi'an kufanya mazoezi. Bw. Zhang mwenye umri wa miaka 80 ni mkazi wa mji wa Xi'an. Alisema,

    "Katika bustani hiyo kuna vifaa mbalimbali vya mazoezi ya kujenga mwili. Kila siku ninakuja hapa kufanya mazoezi. Hii ni mara yangu ya pili kuja hapa kwa leo. Asubuhi nakuja kutumia vifaa vya mazoeiz, na alasiri nakuja kutembea."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako