• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto yapungua kwa asilimia 50 katika nchi saba zilizoko kusini mwa Sahara

    (GMT+08:00) 2013-08-05 15:49:20

    Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni imeonesha kuwa, tangu mwaka 2009 maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa watoto wa Afrika, huku nchi saba zilizoko kusini mwa Sahara zikiwa zimepunguza kiwango cha maambukizi kwa asilimia 50. Kwa mujibu wa ripoti hiyo inayohusu Mpango wa Dunia wa kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa watoto kabla ya mwaka 2015 na kuhakikisha mama zao wanakuwa hai, nchi hizo saba ni pamoja na Botswana, Ethiopia, Ghana, Malawi, Namibia, Afrika Kusini na Zambia.

    Lakini Pili licha ya nchi hizo, nyingine mbili zinazojitahidi kufikia kiwango hicho katika kupunguza maambukizi ambapo pia zimepata maendeleo makubwa ni Tanzania na Zimbabwe. Mpango huo unaongozwa na shirika la UNAIDS, pamoja na Mpango wa dharura wa rais wa Marekani wa kupunguza kiwango cha maambukizi ya UKIMWI ambao ulizinduliwa mwezi Juni mwaka 2011, una malengo mawili muhimu: kwanza ni kupunguza kwa asilimia 90 kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa watoto, na kupunguza kwa asilimia 50 vifo vya kinamama wakati wanapojifungua.

    Mpango huo unazihusisha nchi 22 ambazo maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto yanachukua asilimia 90 ya maambukizi yote. Ripoti hiyo imeonesha maendeleo yaliyopatikana katika nchi 21 zilizoko kusini mwa Sahara na baadhi ya changamoto zinazokabiliana nazo katika mchakato wa kutimiza malengo yaliyowekwa kabla ya mwaka 2015. Pia imesisitiza kuwa idadi ya watoto walioambukizwa virusi vya UKIMWI imepungua hadi laki 1.3 katika nchi hizo 21 zilizopewa kipaumbelela barani Afrika katika mpango huo, na kiasi hicho kimepungua kwa asilimia 38 tokea mwaka 2009.

    Mkurugenzi mtendaji wa Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu HIV Bw. Michel Sidibe amesema, maendeleo yanayopatikana katika nchi nyingi za Afrika ni dalili kubwa kuwa, kukiwa na juhudi za makini, kila mtoto ataweza kuzaliwa bila ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI. Lakini Sidibe pia ameeleza kuwa, maendeleo hayo yamekwamia katika baadhi ya nchi kutokana ambapo bado zina kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI, hivyo amesisitiza kuwa kuna haja ya kujua chanzo cha hali hiyo na kuondoa vikwazo vilivyopo.

    Wakati huo huo ripoti hiyo imeeleza kuwa, idadi ya watoto wanaohitaji matibabu ya UKIMWI itapungua kama kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kitapungua, hivyo hatua za lazima zinatakiwa kuchukuliwa ili kuboresha matibabu ya UKIMWI katika hatua ya mwanzo kwa watoto, na kuwahakikisha wanapewa matibabu ya ARVs kwa wakati. Zaidi ya hayo, ripoti hiyo pia imeonesha kuwa watoto watatu kati ya 10 katika nchi nyingi zinazohusishwa katika Mpango wa Dunia ndio wanaoweza kupatiwa matibabu, hali ambayo imeonesha kuwa kiwango cha watoto wanaopewa matibabu bado kiko chini sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako