• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Uzbekistan wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2013-09-09 19:06:06

    Rais Xi Jinping wa China na rais Abduganiyevich Karimov wa Uzbekistan leo wamefanya mazungumzo, na kubadilishana maoni kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala ya kimataifa na kikanda wanayoyafuatilia.

    Imefahamika kuwa baada ya mazungumzo, marais hao watasaini nyaraka muhimu, na kuhudhuria hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Baada ya kumaliza ziara nchini Uzbekistan, rais Xi Jinping atafanya ziara nchini Kirghizstan, na kuhudhuria mkutano wa 13 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai utakaofanyika mjini Bishkek.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako