• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 1119

    (GMT+08:00) 2013-11-19 19:10:27
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Aaron Thomas wa S.L.P 1805-40200 Kisii Kenya, anaanza kwa kusema nimekuwa nikifuatilia vipindi na matangazo ya CRI tangu nilipokuwa darasa la saba hadi sasa, imekuwa muda mrefu sana kuwa shabiki wa redio toka nilipokuwa na umri wa miaka 15. Nataraji kuwa mimi ndiye shabiki mdogo sana kujisajili katika CRI. Kila mara ninapopokea barua kutoka China huwa ninajawa na furaha tele. Nikikumbuka vizuri nilipokuwa kidato cha tatu nilipokea tuzo ya mshindi wa nafasi ya tatu kwenye shindano la maonesho ya Shanghai.

    Natumai kuwa siku moja nitaweza kuitembelea China kwani hata sauti za kichina zinanipendeza, pamoja na mambo mengine ya Kichina. Baadhi ya rafiki zangu wangependa sana kujiunga na CRI, hii ni kwasababu kila mara wanapoitazama albamu yangu ambayo nimehifadhi picha za kichina wanatabasamu. Pia nimejifunza baadhi ya maneno ya kichina ambayo ni lugha ya kufarahisha sana. Badhi yao huyatumia kwa kuwasalimia watu na kuwashukuru.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Aaron Thomas kwa barua yako, kwanza tunakupa hongera kwa kujiunga na CRI ukiwa mdogo sana. Kuhusu rafiki zako wanaotaka kujiunga na CRI waambie hilo ni jambo linalowezekana kabisa, wanaweza kututumia anuani zao ili tuweze kuwatumia kadi za salamu na zawadi nyingine ndogondogo tunazotoa kwa wasikilizaji wetu, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Kornel I Joseph wa Babati Manyara Tanzania, anasema ninafuraha ya kuandika barua hii fupi kuwaarifu kuwa mimi ni msikilizaji wenu na mpenzi wa redio China. nina kikundi cha watu sita ambao tunasikiliza matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa. Ninawapongeza kwa matangazo hayo na ninafurahi pamoja na kikundi changu. Tunawaomba muendelee kutusaidia haya yafuatayo kwanza ratiba ya matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya CRI, kalenda, magezeti makala ya Kiswahili ya habari za China na sera au misimamo ya China kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa na hasa yale yahusuyo nchi changa kama Tanzania. zamani kidogo wakati nilipokuwa shule ya msingi nililetewa magezeti haya laikini sasa hata anuani yenu nimepoteza. Mwisho nawatakia mafanikio mema na kazi njema.

    Nasi tunakushukuru kwa dahati msikilizaji wetu Kornel I Joseph kwa barua yako fupi, tumesikia maombi yako, na tutajitahidi kukutumia mambo uliyoomba hususan jarida, tutamtaarifu muhusika akutumie jarida la daraja la urafiki ambalo limesheheni habari kemkem zilizoandikwa kwa Kiswahili, pamoja na kalenda ahsante sana.

    Naye msikilizaji wetu Fadhili Juma Makame wa S.L.P 573 Zanzibar anasema naamini kuwa mpo pamoja watangazaji na wasikilizaji. Idadi kubwa ya watu nchini China wana asili ya watu wa Han karibu asilimia 6 ya idadi ya watu wa China hawatoki kabila la Han yaani ni watu wa makabila madogo. Nchini China kuna makabila madogo 54, na kila kabila lina mila na desturi zake na lugha yake, haya yanapatikana zaidi katika maeneo ya mipaka ya China kama vile Tibet na kwengineko.

    Makabila makubwa kati ya 54 ni wamongolia na watibet. Kwa karne nyingi wamongolia wameishi kama wafugaji wa kondoo, farasi na ngamia. Watibet huishi sana katika mkoa wa Sichuan, Qinghai na Xizang, na pia wengi wao ni wakulima. Wasikilizaji na watangazaji wapendwa hayo ni mawazo na maoni yangu kuhusu haya makabila ambayo yamepewa kipaumbele sana na serikali.

    Tunapenda kukushukuru sana msikilizaji wetu Fadhili Juma Makame kwa barua yako na pia tunakupongeza kwa kufuatilia mambo ya makabila ya kiutamaduni ya China, na pia kujua historia ya China, asante sana.

    Sasa tunawaletea ujumbe tuliotumiwa na wasikilizaji wetu kwenye tovuti yetu na kwanza ni msikilizaji wetu Bett Geoffrey baruapepe yake ni bettchergeff@gmail.com sanduku la posta 13, Bomet Kenya-Nairobi anasema ningependa kuwapongeza watangazaji wa redio China Kimataifa kwa jukumu lenu wakati wote; Salamu zangu zinaenda kwa wazikilizaji wote duniani ambao wanasikiliza CRI idhaa ya Kiswahili. Ni kweli napata kuelimishwa na kuburudishwa, sana hapa Redio China.. Moses, Fundi Bengo, Pili Mwinyi miongoni wa wengineo. Suntururu au ukipenda Sheshe.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu wote mliotutumia ujumbe kupitia kwenye tovuti yetu, tunawaomba tu muendelee kutembelea mtandao wetu na kusikiliza matangazo kwenye redio ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako